Pata taarifa kuu
LIBYA-SHERIA-BUNGE-Uchaguzi-Siasa

Libya: Mahakama kuu yachukua uamzi wa kutolitambua Bunge la Tobruk

Mahakama kuu imechukua uamzi leo Alhamisi Novemba 6 wa kutolitambua Bunge liliyotokana na uchaguzi uliyofanyika Juni 25 mwaka 2014, lenye makao yake makuu  mji mjini Tobruk, mashariki mwa Libya.

Maandamano ya furaha mbele ya makao makauu ya Mahakama kuu mjini Tripoli, baada ya uamzi wa kutolitambua Bunge liliyotokana na uchaguzi wa mwezi Juni lenye makao makuu Tobruk, Alhamisi novemba 6 mwaka 2014.
Maandamano ya furaha mbele ya makao makauu ya Mahakama kuu mjini Tripoli, baada ya uamzi wa kutolitambua Bunge liliyotokana na uchaguzi wa mwezi Juni lenye makao makuu Tobruk, Alhamisi novemba 6 mwaka 2014. REUTERS/Ismail Zitouny
Matangazo ya kibiashara

Mahakama kuu imechukua uamzi leo Alhamisi Novemba 6 wa kutolitambua Bunge liliyotokana na uchaguzi uliyofanyika Juni 25 mwaka 2014. Makao makuu ya Bunge hilo yako katika mji wa Tobruk, mashariki mwa Libya.
Bunge hilo limekua likitambuliwa na Jumuiya ya kimataifa. Uamzi wa mahakama kuu wa kutolitambua Bunge hilo la Tobruk umezua mtafaruku.

Mahakama kuu imechukua uamzi wa kupinga Bunge hilo lenye makao yake Tobruk, mashariki mwa Libya, ambalo linaundwa kwa idadi kubwa ya Wabunge ambao si Waislam wenye itikadi kali za kidini. Kwa mujibu wa Mahakama kuu hiyo, utaratibu uliyopelekea kufanyika kwa uchaguzi Juni 25 ulikua kinyume na Katiba.

Mahakama kuu bado haijahalalisha uamuzi wake. Matokeo ya tangazo hili bado hayajawekwa wazi lakini yanaweza kusababisha kuvunjwa kwa Baraza la Wawakilishi.

Kutokana na uamzi huo Bunge la kitaifa lenye makao yake mjini Tripoli ndilo lenye majukumu kwa sasa, licha ya kuwa muhula wake ulimalizika na uchaguzi wa mwezi Juni. hata hivyo, Bunge hili la kitaifa liliyomaliza muhula wake mwezi Juni, kulingana na jinsi Katiba inavyoeleza, linapaswa kuandaa upya uchaguzi. Hali hiyo inamaanisha kuwa maazimio yaliyopitishwa na Bunge la Tobruk yamekwenda kombo.

Mmoja kati ya wasemaji wa Bunge la Tobruk, amesema hawakubaliani na uamzi huo wa Mahakama kuu, akibani kwamba Mahakama hiyo imechukua uamzi wa kutolitambua bunge la Tobruk kutokana na vishawishi inayopata kutoa kwa jeshi na wanamgambo wa kiislam ambao wanadhibiti kwa sasa mji wa Tripoli.

Wakati huo huo Bunge la zamani la kitaifa lenye makao yake Tripoli limepongeza uamzi huo. Wakaazi wa mji wa Tripoli wamedhihirisha furaha yao kwa kuandamana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.