Ushairi ni sanaa inayokua kila kukicha na watunzi wamekua na maana mbalimbali kuhusu ushairi, Senkoro (1988) Katika kitabu chake cha Ushairi, “Nadharia na Tahakiki” anasema ni utanzu wa fasihi utumiao mpangilio wa lugha ya mkato, picha, iliyopangwa kwa njia iletayo mapigo mahususi au yaliyomo ndani yake.Wamitila, (2008) ushairi ni utungo wa sanaa ya lugha na mpangilio maalum wa mishororo, ama kisauti na kwa maneno mateule kwa kubuni mbinu za lugha zenye mnato na mbinu nyingine za kibalagha na kimtindo zinamwezesha mtunzi kuwasilisha ujumbe kwa kifupi na kwa mkokotezo mkubwa unaoelezea hisia, tukio, ama hali kwa lugha ya mvuto.Kwa ujumla ushairi ni sanaa ya lugha ya mkato yenye ughunaji inayosawiri, kueleza au kuonesha jambo, hisia au katika mpangilio mahususi wa maneno wenye urari wa vina na wizani wa sauti.Kutana na Mariagoreth Charles Msanii wa kughani Mashairi kutoka Tanzania akizungumza na Steven Mumbi katika Makala haya.
Vipindi vingine
-
20:05
-
Tanzania: Sanaa ya uigizaji, tunamuangazia Asha Jumbe maarufu White Maria
Asha Jumbe maarufu White Maria ni Muigizaji aliyejizolea umaarufu akiwa na umri wa Miaka nane tu, sasa ni mtu Mzima aja kivingine kufanya sanaa ya Fimalu za kiswahili,Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumzia safari yake ya Uigizaji.11/05/202420:12 -
Wiki hii makala haya yanamuangazia Steven Ibrahim maarufu Eddy Music
Sanaa ya Muziki imenihitaji kuliko nilivyo ihitaji, ni kauli yake Steven Ibrahim maarufu Eddy Music alipozungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.04/05/202420:03 -
Muziki wa injili na Obby Alpha ambaye ametunga vibao kama bora kushukuru
Msani huyo amesema kuwa alitunga vibao kama bora kushukuru kutokana na changamoto za kimaisha alizokuwa anakabiliwa nazo kipindi fulani katika maisha yake.27/04/202420:02 -
Zanzibar: Fahamu zaidi kuhusu Muziki wa Baibuda katika makala haya
Mwandishi wetu Steven Mumbi amezungumza na msani wa muziki huu wa Baibuda13/04/202420:09