Pata taarifa kuu

Uturuki: zaidi ya watu 200 walikamatwa Istanbul kando ya Siku ya Wafanyakazi

Waandamanaji zaidi ya 200 waliokusanyika Istanbul kusherehekea Mei 1 wamekamatwa leo Jumatano na polisi, waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP wamebaini.

Wanachama wa vyama vya wafanyakazi wakikabiliana na polisi wa kutuliza ghasia wa Uturuki wakati wa Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi, Jumatano hii, Mei 1, 2024 mjini Istanbul.
Wanachama wa vyama vya wafanyakazi wakikabiliana na polisi wa kutuliza ghasia wa Uturuki wakati wa Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi, Jumatano hii, Mei 1, 2024 mjini Istanbul. AP - Khalil Hamra
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano ya kwanza yalizuka wakati waandamanaji walipojaribu kuvunja vizuizi vya polisi kufika kwenye uwanja wa Taksim Square, kitovu cha maandamano katikati ya jiji kuu la Uturuki.

Askari polisi 42,000 wahamasishwa

Istanbul ilizingirwa na vikosi vya usalama vilivyofunga eneo la katikati mwa mji mkuu wa Uturuki. Zaidi ya maafisa wa polisi 42,000 wametumwa katika jiji hilo kuu, Waziri wa Mambo ya Ndani Ali Yerlikaya alionya Jumanne, akikashifu mapema "mashirika ya kigaidi (yanayotaka) kuifanya Mei 1 kuwa uwanja wa hatua na propaganda."

Kuanzia kingo za Bosphorus hadi peninsula ya kihistoria ya Sultanhamet na Jumba la Topkapi, vizuizi vya chuma vinazuia njia zote, usafiri wa umma, pamoja na feri, zimefungwa, hali ambayo imesababisha watalii kunaswa ambao huburuta masanduku yao chini ya anga yenye kiza.

Kuanzia asubuhi, wakati waandamanaji walikusanyika katika wilaya ya Besiktas kusherehekea Mei 1, matukio yalizuka na maafusa wa polisi na watu kadhaa walichukuliwa bila kujali kuingizwa katika gari za polisi. Mkusayiko mwingine, ulioitishwa mbele ya manispaa ya Istanbul na meya wa upinzani Ekrem Imamoglu na chama chake, CHP, pia ulizuiwa kusonga mbele.

"Taksim ni ya wafanyakazi"

Akizungumza pamoja na Meya, ambaye kwa kiasi kikubwa alichaguliwa tena Machi 31, kiongozi wa CHP, chama kikuu cha upinzani bungeni, Özgür Özel ameahidi "kutokata tamaa": "Tutaendelea na juhudi zetu hadi Taksim iwe huru". “Taksim ni ya wafanyakazi,” amesema, kisha kuwaambia maafisa wa polisi: “Wafanyakazi hawa si maadui zenu tu. Tunachotaka ni kwamba siku hii iadhimishwe kama sikukuu. hatutaki mgogoro".

Mikusanyiko haijaidhinishwa tena katika Taksim Square, ambayo imekuwa kitovu cha cmaandamano kwa mamlaka ya Recep Tayyip Erdogan tangu wimbi la maandamano ambayo yalitikisa nchi hiyo mwaka 2013. Lakini vyama vya wafanyakazi na vyama vya kisiasa mara kwa mara vinatoa wito kwa wanachama wao kukusanyika katika uwanja huo. Jumanne jioni, Mkuu wa Nchi alishutumu "makundi ya kigaidi ambayo yanataka kuifanya Mei 1 kuwa chombo cha propaganda" na kuonya vyama vya wafanyakazi na vyama vya kisiasa dhidi ya "hatua yoyote ambayo itadhuru mazingira ya Mei 1".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.