Pata taarifa kuu

Kifo cha Navalny: Shinikizo la nchi za Magharibi laongezeka dhidi ya Moscow

Baada ya kutangazwa kwa kifo cha Alexei Navalny, kiongozi mkuu wa upinzani wa Urusi na mkosoaji mkuu wa Kremlin, ambaye alifariki akiwa gerezani katika mazingira ambayo bado hazijajulikana, mvutano unaendelea kuongezeka. Nchi za Magharibi zinawaita mabalozi wa Urusi kwa zamumara kwa mara na kutishia kuchukua vikwazo vipya dhidi ya Moscow.

Waandamanaji wakiandamana mbele ya ubalozi wa Urusi mjini Berlin mnamo Februari 18, 2024.
Waandamanaji wakiandamana mbele ya ubalozi wa Urusi mjini Berlin mnamo Februari 18, 2024. © REUTERS - ANNEGRET HILSE
Matangazo ya kibiashara

 

Baada ya London, ambayo ilikuwa imewaita wanadiplomasia kutoka ubalozi wa Urusi siku ya Ijumaa jioni, kuwafahamisha kwamba mamlaka ya Urusi itawajibishwa "kikamilifu" kwa kifo cha mpinzani namba moja wa Kremlin, Jumatatu hii serikali kadhaa za Ulaya zilifanya hivyo.

Berlin kwanza, ikifuatiwa na Stockholm ambayo pia ilichukua hatua katika ngazi ya Ulaya kuchunguza uwezekano wa vikwazo vipya dhidi ya Moscow. Madrid,  Hague, Oslo kisha Paris walifuata mkondo huo, kuwaita mabalozi wa Urusi wa nchi husika, kuwaomba ufafanuzi juu ya kifo cha Alexei Navalny, ambaye mwili wake bado haujakabidhiwa kwa familia wala kwa washirika wake wa karibu.

Hali hiyo iimeendelea kuwa ngumu mjini Brussels ambapo mkuu wa diplomasia ya Ulaya Josep Borrell alionya, baada ya kukutana na mjane wa mpinzani wa Urusi, kwamba Vladimir Putin itabidi "awajibike" kwa kifo cha Navalny. Mwishoni mwa mkutano na mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya (EU), nchi Ishirini na Saba wanachama wa Umoja wa Ulaya walitoa wito wa "uchunguzi huru na wa uwazi wa kimataifa kuhusu mazingira ya kifo hiki cha ghafla".

Hatimaye, huko Washington, Rais wa Marekani Joe Biden amesema anazingatia vikwazo vipya dhidi ya Urusi, ambavyo vitaongezwa kwenye mlolongo wa vikwazo ambavyo tayari vimetumika dhidi ya Moscow tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 24, 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.