Pata taarifa kuu

Uingereza: Mfalme Charles wa tatu amepatikana na saratani

Nairobi – Nchini Uingereza Kasri ya Buckingham imetangaza kuwa Mfalme Charles wa tatu amepatikana na saratani.

Kasri ya Buckingham imesema Mfalme ameanza matibabu na ataahirisha baadhi ya kazi zake za kila siku
Kasri ya Buckingham imesema Mfalme ameanza matibabu na ataahirisha baadhi ya kazi zake za kila siku AFP - ADRIAN DENNIS
Matangazo ya kibiashara

 

Hata hivyo, taarifa hazijasema ni aina gani ya saratani inayomsumbua Mfalme Charles wa tatu, lakini ripoti zinasema kuwa iligundulika wakati alipokwenda kufanyiwa matibabu ya kuongezeka kwa tezi dume.

Kasri ya Buckingham imesema Mfalme ameanza matibabu na ataahirisha baadhi ya kazi zake za kila siku.

Aidha, taarifa hiyo imesema, Mfalme Charles wa tatu mwenye umri wa miaka 75 , amesema  ana matumaini makubwa kuwa hali yake itaimarika na atarejelea shughuli zake za kila siku, hivi karibuni.

Hata hivyo, haijaelezwa yupo katika hatua gani ya saratani. Inatarajiwa kuwa ataendelea kukutana ana kwa ana kila wiki na Waziri Mkuu Rishi Sunak kujadili masuala muhimu ya serikali, iwapo madaktari hawatokuwa na pingamizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.