Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Baraza Kuu la UN lataka 'kuondoka mara moja' kwa wanajeshi wa Urusi

Katika azimio hili lisilo la kisheria lililopitishwa na idadi kubwa ya wajumbe katika mkesha wa kuadhimisha mwaka wa kwanza wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa pia limetoa wito wa amani "ya haki na ya kudumu".

Azimio hilo lilipitishwa kwa kura 141 dhidi ya 7, huku nchi 32 zikijizuia. New York, Alhamisi, Februari 23, 2023.
Azimio hilo lilipitishwa kwa kura 141 dhidi ya 7, huku nchi 32 zikijizuia. New York, Alhamisi, Februari 23, 2023. AP - Bebeto Matthews
Matangazo ya kibiashara

Azimio hilo lisilo la kisheria limepitishwa kwa kura 141 dhidi ya 7 (Urusi, Belarus, Syria, Korea Kaskazini, Mali, Nicaragua, Eritrea) na nchi 32 hazikupiga kura, zikiwemo China na India, kati ya nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa. Uungwaji mkono kama huo mnamo mwezi Oktoba mwaka jana, wakati nchi 143 zililaani kunyakuliwa kwa maeneo kadhaa ya Ukraine na Urusi, tano zilipinga.

Azimio lililopitishwa linathibitisha tena "ahadi" kwa "uadilifu wa eneo la Ukraine" na "linataka" kwamba Urusi "mara moja, kabisa na bila masharti majeshi yake yote yaondoke bila kuchelewa katika maeneo ya Ukraine ndani ya mipaka inayotambuliwa kimataifa ya nchi", likimaanisha maeneo yalichukuliwa na Urusi. Pia linataka "kusitishwa kwa uhasama" na "linasisitiza haja ya kufikia, haraka iwezekanavyo, amani ya kina, ya haki na ya kudumu nchini Ukraine kwa mujibu wa kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa".

Kwa mwaka mmoja, wakati Urusi imekuwa ikitumia haki yake ya kura ya turufu kuzuia hatua zozote katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukraine, Baraza Kuu limechukua nafasi hii kuionya Urusi.

Tangu Jumatano, wawakilishi wa makumi ya nchi wameandamana hadi kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa kuunga mkono Ukraine, wakati Kyiv ikiwahimiza wanachama wa jumuiya ya kimataifa kuchagua kati ya "mema na mabaya". "Baada ya mwaka mmoja, hatupaswi kukutana kuadhimisha mwaka wa pili wa vita hivi vya kipuuzi vya uchokozi," alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani Yoshimasa Hayashi

Wkati huo huo Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema Ukraine haijashindwa na imepambana na vizingiti vingi na kwamba itashinda dhidi ya uvamizi wa vikosi vya Urusi.

Akizungumza Alhamisi, siku moja kabla ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu Urusi ilipoivamia Ukraine Februari 24, Zelensky amesema watawawajibisha wale wote ambao wamesababisha uovu huo katika ardhi yao.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.