Pata taarifa kuu

Athari za vita vya Ukraine kwa uchumi na siasa za bara Afrika

NAIROBI – Uvamizi wa Ukraine unapotumia mwaka moja leo, umekuwa na athari kubwa kwa bara la Africa ambalo bado lilikuwa linashuhudia athari za janga la uviko 19.Benson Wakoli anathimini kwa kina athari ya vita hivyo.

Vita vya Ukraine vimeonekana kuathiri pakubwa uchumi wa bara Afrika
Vita vya Ukraine vimeonekana kuathiri pakubwa uchumi wa bara Afrika © MARKO DJURICA / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Vita hivyo vya Ukraine vimebabisha tofauti za kisiasa miongoni mwa mataifa ya Afrika, nchi kama Eriterea, Mali na Jamhuri ya Africa ya kati vikiunga mkono uvamizi huo, mengine yamelaani  huku mengine yakionekana kutounga mkono upande wowote.

Vita vya Ukraine pia vimekuwa na athari kubwa ya kiuchumi kwa mataifa ya  Africa, ambapo kampuni nyingi za Urusi zimesitisha shughuli zake hapa Afrika kutokana vikwazo vya kimataifa ambavyo Urusi imewekewa, hili likitikisa uchumi wa baadhi ya mataifa, mfano ukiwa taifa la Equatorial Guinea.

Swala jingine ni kuhusiana na kupanda kwa bei ya vyakula barani Afrika kutokana na vita vya Ukraine, hasa ikizingatiwa kwamba Ukraine na Urusi ni mataifa yaliotegemewa sana kwa usambazaji wa ngano duniani, mataifa kama vile Uganda, Tanzania na Sudan yakiagiza nusu ya ngano yake kutoka Ukraine na Urusi. Swala alilosistizia rais wa Tanzania  samia Suluhu Hassan.

Katika hatua nyingine wafadhili wa kimataifa ambao walihusika katika miradi ya maendeleo kwa mataifa ya Afrika, sasa wameelekeza nguvu zote kumaliza vita hivi vya Ukraine, na huenda hili likasabisha mzozo katika mataifa mengi ya Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.