Pata taarifa kuu

EU yapanga kuanzisha kazi ya mafunzo ya jeshi la Ukraine

Msaada wa kijeshi wa Ulaya kwa Ukraine hivi karibuni unaweza kuchukua fomu ya kazi ya mafunzo kwa jeshi la Ukraine. Hakuna kilichoamuliwa kwa sasa, lakini wazo hilo linatetewa wazi na Tume ya Ulaya. Uongozi wa Umoja wa Ulaya, EU, unataka kutoa mafunzo na usaidizi kwa jeshi la Ukraine katika vita ambavyo vinaonekana kudumu kwenye mipaka ya Muungano.

Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya anayesimamia Sera ya Kigeni, Josep Borrell, huko Brussels mnamo Agosti 18, 2022.
Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya anayesimamia Sera ya Kigeni, Josep Borrell, huko Brussels mnamo Agosti 18, 2022. AP - Virginia Mayo
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Josep Borrell, ujumbe huu wa kijeshi utapanua, kwa kiwango cha Ulaya, msaada wa nchi mbili ambao tayari umetolewa na baadhi ya mataifa wanachama ambayo yameipa Ukraine vifaa vya kijeshi na mafunzo katika matumizi yake. Kwa upande wa Mwakilishi Mkuu wa EU anayesimamia Sera ya Kigeni, kazi hii imeanzishwa kufuatia mzozo wa Ukraine.

"Inaonekana ni jambo la busara kwamba vita vinavyoendelea na ambavyo vinaonekana kuwa vya kudumu vinahitaji juhudi sio tu katika suala la usambazaji wa vifaa, lakini pia mafunzo na kusaidia kupanga jeshi," na hilo ndilo linalojadiliwa kati ya nchi wanachama, amethibitisha Josep. Borrell. Hili litakuwa mada ya mjadala wa kisiasa Jumatatu ijayo huko Prague katika kikao cha Baraza la Mawaziri wa Ulinzi. Na natumai itaidhinishwa."

Maelezo ya uwezekano huu wa kupelekwa kikosi nchini Ukraine kwa siku zijazo bado hayajajulikana. haijulikani fomu halisi itakuwaje au ni wanajeshi wangapi wa Ulaya  watapelekwa, hii itakuwa sehemu ya mazungumzo kati ya nchi wanachama. Kilicho hakika ni kwamba Umoja wa Ulaya hautaingilia moja kwa moja katika uwanja wa vita, Josep Borrell amehakikisha. Usaidizi na mafunzo yatafanyika katika nchi jirani za Ukraine, ili Umoja wa Ulaya usionekane kama mshirika wa vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.