Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Latvia yaitangaza Urusi kuwa 'nchi ya kigaidi'

Hii imeamuliwa na wajumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Latvia. Tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Latvia imeunga mkono Kyiv kwa kuipa vifaa vya kijeshi, lakini pia kwa kuchukua msimamo.

Kamati ya Masuala ya Kigeni ya Bunge la Latvia imetangaza hivi punde tu kwamba Urusi ni taifa la kigaidi katika taarifa. Hapa kwenye picha ni makao maku ya Bunge la Latvia, Januari 2021.
Kamati ya Masuala ya Kigeni ya Bunge la Latvia imetangaza hivi punde tu kwamba Urusi ni taifa la kigaidi katika taarifa. Hapa kwenye picha ni makao maku ya Bunge la Latvia, Januari 2021. AFP - GINTS IVUSKANS
Matangazo ya kibiashara

Urusi ni "nchi ya kigaidi". Hivi ndivyo wajumbe wa Kamati ya Mambo ya Kigeni ya Bunge la Latvia wameielezea Urusi katika taarifa. Mashambulizi ya kijeshi yaliyolengwa na Urusi dhidi ya raia na maeneo ya umma nchini Ukraine ni ugaidi, na Urusi ni mfadhili wa ugaidi.

Akihojiwa na RFI, Rihards Kols, mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, anatumai kuwa Bunge litaidhinisha nakala hii kwa kauli moja. "Kama maamuzi yote yaliyochukuliwa na Latvia kuunga mkono Ukraine tangu Februari 24," alisema.

Warusi wako chini ya udhibiti mkali kwenye mipaka ya Latvia. Idara ya Usalama ya Latvia ilitangaza mapema Julai kwamba imekataa kuingia nchini humo kwa raia 53 wa Shirikisho la Urusi, pamoja na mambo mengine, kwa sababu wanaunga mkono uvamizi wa kijeshi wa Urusi nchini Ukraine.

Lakini Riga inataka kwenda mbali zaidi. inauomba Umoja wa Ulaya kusitisha kutoa viza kwa Warusi, iwe kwa utalii, kazi au masomo. hatua ambayo tayari imepitishwa na Estonia, ambayo inatarajia kutangazia suala hili katika Umoja wa Ulaya mwishoni mwa mwezi Agosti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.