Pata taarifa kuu

Mgogoro wa Ukraine : Marekani yadai uvamizi wa Urusi unakaribia, Moscow yakanusha

Hatari ya uvamizi wa Urusi dhii ya Ukraine iko kwenye kiwango cha "juu" ametangaza Rais wa Marekani Joe Biden Alhamisi Februari 17. Urusi inakanusha, lakini inatishia "kuchukuwa hatua" kama Marekani itaendelea kufutilia mbali matakwa yake ya usalama.

Mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Belarus na Urusi karibu na mji wa Brest (Belarus), Februari 16, 2022.
Mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Belarus na Urusi karibu na mji wa Brest (Belarus), Februari 16, 2022. - Russian Defence Ministry/AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulio linawezekana "katika siku zijazo", rais wa Marekani ametaka kutahadharisha mbele ya waandishi wa habari kabla ya kuondoka Ikulu ya White House kwa ziara ya saa chache kuelekea Ohio. Joe Biden amesema "hakupanga" kumpigia simu mwenzake wa Urusi Vladimir Putin. "Dalili zote tulizo nazo ni kwamba wako tayari kuingia Ukraine, kushambulia Ukraine," ameongeza.

Kufikia sasa, rais alikuwa ameonya mara kwa mara dhidi ya hatari ya uvamizi, lakini amebaini kwamba Vladimir Putin aikuwa bado hajachukuwa uamuzi. Washington imeongeza kwa uwazi sana kiwango cha tahadhari kwa saa chache na kuhakikisha kwamba Urusi, mbali na kuwaondoa wanajeshi kwenye mpaka wa Ukraine kama ilivyoahidi, kinyume chake imeendelea kuimarisha kikosi chake na kuongeza idadi ya askari kwenye mpaka na Ukraine. Marekani pia inaonya dhidi ya kuongezeka kwa uongo na kisingizio kutoka Moscow, ambavyo vinaweza kutumika kama sababu ya uvamizi.

Kwa upande wake, Urusi imesisitiza tena Alhamisi kutozingatia uvamizi wowote dhidi ya Ukraine licha ya kutumwa kwa wanajeshi zaidi ya 100,000 wa Urusi kwenye mipaka ya Ukraine, jambo ambalo linazifanya nchi za Magharibi kuogopa operesheni ya kijeshi inayokaribia dhidi ya Kiev.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.