Pata taarifa kuu

Ukraine: Washington yalaani wito wa Duma kutambua uhuru wa maeneo yaliyojitenga

Urusi kutambua uhuru wa maeneo yaliyojitenga nchini Ukraine ni "ukiukaji mkubwa wa sheria ya kimataifa", ameshutumu Jumatano Februari 16 Waziri wa Mmbo ya Nje wa Marekani Antony Blinken.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken wakati wa akijadili kuhusu hali kati ya Urusi na Ukraine, Januari 26, 2022 huko Washington.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken wakati wa akijadili kuhusu hali kati ya Urusi na Ukraine, Januari 26, 2022 huko Washington. © 2019 AFP
Matangazo ya kibiashara

Bunge la Urusi lilipigia kura siku ya Jumanne wiki ombi la Rais Vladimir Putin ili Urusi iweze kutambua uhuru wa maeneo yanayoiunga mkono Mosco ambayo yamekuwa yakipigana, kwa msaada wake, na jeshi la Ukraine mashariki mwa nchi hiyo kwa miaka minane.

"Utekelezaji wa azimio hili utadhoofisha zaidi mamlaka na uhuru wa Ukraine," ameshutumu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani katika taarifa. Pia "itatilia shaka zaidi ahadi ya Urusi ya kuendelea kushirikiana kidiplomasia ili kufikia utatuzi wa amani" wa mgogoro wa mpaka na Ukraine, amesema Antony Blinken. Ameonya zaidi kwamba Moscow itajikuta imekabiliwa vikali "kwa hatua za haraka na thabiti kutoka kwa Marekani kwa uratibu wa karibu" na washirika wake.

Kwa hivyo Marekani inajiunga na Umoja wa Ulaya ambao tayari ulikuwa "umelaani vikali" wito wa Bunge la Urusi (Duma) siku ya Jumanne, kupitia sauti ya mkuu wa sera za Umoja wa Ulaya Josep Borrell.

Maeneo yaliyojitangaza kujitawala na ambazo zinaunga mkono Urusi ya Donetsk na Lugansk yamekuwa yakipigana, kwa msaada wa Moscow, na jeshi la Ukraine mashariki mwa Ukraine kwa miaka minane. Mzozo huu, ambao ulizuka baada ya urusi kuikalia kimabavu jimbo la Crimea, umesababisha vifo vya zaidi ya watu 14,000 tangu mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.