Pata taarifa kuu
UFARANSA-USALAMA

Watatu wauawa katika shambulio la kisu Nice

Watu watatu wameuawa leo Alhamisi asubuhi katika shambulio lililotokea katika kanisa la Notre-Dame huko Nice, Kusini mwa Ufaransa, na wengine kadhaa wamejeruhiwa, msemaji wa polisi wa ametangaza.

Watu wawili waliuawa asubuhi ya Alhamisi hii, Oktoba 29, katika shambulio la kisu karibu na kanisa la Notre-Dame huko Nice, Kusini mwa Ufaransa.
Watu wawili waliuawa asubuhi ya Alhamisi hii, Oktoba 29, katika shambulio la kisu karibu na kanisa la Notre-Dame huko Nice, Kusini mwa Ufaransa. REUTERS/Eric Gaillard
Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji alijeruhiwa na kukamatwa, kulingana na msemaji wa polisi. Ofisi ya mashtaka dhidi ya ugaidi iliombwa kuanzisha uchunguzi.

Mmoja kati ya watu hao watatu waliouawa, alichinjwa, na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio hilo la kisu. Mshambuliaji kwa sasa yuko mikononi mwa polisi, kulingana na ripoti mpya kutoka kwa chanzo cha polisi. Watu wawili, mwanamume na mwanamke, waliuawa katika kanisa la Notre-Dame na wa tatu, aaliyekuwa amejeruhiwa vibaya, alifariki katika baa moja alikokuwa amekimbilia.

Ofisi ya mashtaka dhidi ya Ugaidi (Pnat) imefungua uchunguzi wa "mauaji na jaribio la mauaji kwa ushirikiano na kundi la kigaidi" na "kundi la magaidi wahalifu".

Wakati huo Waziri wa Mambo ya Ndani, Gérald Darmanin, ameongoza "mkutano wa dharua" huko Paris. Naye rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amezuru eneo la shambulio akiambana na Meya wa mji wa Nice.

ais wa Ufaransa Emmanuel Macron amezuru eneo la shambulio akiambana na Meya wa mji wa Nice.
ais wa Ufaransa Emmanuel Macron amezuru eneo la shambulio akiambana na Meya wa mji wa Nice. REUTERS/Eric Gaillard/Pool

Hayo yanajiri wakati Rais Emmanuel Macron alisema jana kwamba Ufaransa huenda ikaanza kupunguza vikwazo vya kukabiliana na Corona pale maambukizi ya virusi vya corona yatakapoanza kupungua na kufikia 5,000 kwa siku badala ya idadi ya hivi sasa ya maambukizi 40,000 kwa siku moja.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanataraji kutkutana leo kwa mkutano wa njia ya video kujadili namna ya kuudhibiti mgogoro huo wa virusi vya corona, kulingana na vyanzo vya Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.