Pata taarifa kuu
UFARANSA-CORONA-AFYA

COVID: Ufaransa yajiandaa kwa "maamuzi magumu", hotuba ya Macron Jumatano

Ufaransa inajiandaa kuimarisha hatua zake za kuzuia mlipuko mpya wa janga la COVID-19, hali ambayo huenda makataa ya raia kutotembea yakachukuliwa. Ufaransa imerekodi vifo vipya 523 katika muda wa muda wa saa 24, baada yavifo 266 kuripotiwa siku moja kabla, mamlaka ya afya ilitangaza Jumanne wiki hii.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akihutubia taifa, Machi 16, 2020.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akihutubia taifa, Machi 16, 2020. AFP/Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne, Waziri Mkuu, Jean Castex, amesema ni "muhimu" kuchukuliwa "hatua mpya" "kukabiliana dhidi ya janga la COVID-19,

Waziri Mkuu Castex anatarajia kuwasilisha hatua hizo mpya bungeni Alhamisi wiki hii. "Lazima tuhamasishe sio tu wawakilishi katika ngazi ya kitaifa lakini nchi yetu yote", Waziri Mkuu wa Ufaransa ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Jumanne asubuhi, Emmanuel Macron aliongoza kikao cha kwanza cha baraza la ulinzi, kikao ambacho alishiriki Waziri Mkuu na mawaziri kadhaa, ikiwa ni ufunguzi wa mfululizo wa mikutano ambayo itaendelea hadi Jumatano.

Emmanuel Macron atatoa hotuba kwa njia ya televisheni Jumatano hii saa mbili usiku kutangaza hatua mpya za kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona, ikulu ya Elysée ilibaini Jumanne wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.