Pata taarifa kuu
UFARANSA-CORONA-AFYA

Maambukizi ya virusi vya Corona yashika kasi Ufaransa

Idadi ya maambukizi haijatisha sana, lakini inaonekana kuwa virusi vya Corona vinashika kasi katika baadhi ya majimbo nchini Ufaransa. Kwa kawaida, viongozi wa afya wanajikita kuangalia kila wakati R0, kipimo kinachowezesha kuangalia kasi ya kusambaa kwa virusi.

Virusi vinaendelea kushika kasi haraka katika maeneo manne ya Jimbo la Bretagne, ambapo mgonjwa wa Covid-19 anaweza kuambukiza watu zaidi ya wawili (2.6). Kesi mpya 110 ziliripotiwa katika siku tano tu. hapa ni Nice.
Virusi vinaendelea kushika kasi haraka katika maeneo manne ya Jimbo la Bretagne, ambapo mgonjwa wa Covid-19 anaweza kuambukiza watu zaidi ya wawili (2.6). Kesi mpya 110 ziliripotiwa katika siku tano tu. hapa ni Nice. VALERY HACHE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika mikoa mingine, virusi vya Corona vimeongezeka. Jimbo la Bretagne ndilo linatsha zaidi. R0, idadi ya wastani ya watu walioambukizwa na mtu mmoja mwenye virusi vya Corona, sasa imefikia 2.6 kulingana na takwimu kutoka idara ya afya ya umma nchini Ufaransa. Wiki iliyopita ilikuwa 1.07.

Virusi vinaendelea kushika kasi haraka katika maeneo manne ya Jimbo la Bretagne, ambapo mgonjwa wa Covid-19 anaweza kuambukiza watu zaidi ya wawili (2.6). Kesi mpya 110 ziliripotiwa katika siku tano tu.

Mikoa ya Provence-Alpes-Côte d'Azur na Reunion pia ina kiwango cha kuzaliana kwa virusi ambacho kimefikia kwenye mstari mwekundu.

Nchini kote Ufaransa, R0, imeendelea kuwa kwenye kiwango cha chini : kiko kwenye 1.18, lakini bado ni kitisho, hata kama inamaanisha kuwa janga hilo halijasumbua kama ilivyokuwa wiki mbili zilizopita.

Madaktari na mamlaka ya afya wameendelea kusema: kuwa ni lazima watu wawe makini sana na kuheshimu masharti yaliyowekwa kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19.

Uvaaji wa barakoa utakuwa ni lazima katika maeneo ya umma nchini Ufaransa kuanzia Jumatatu wiki ijayo. Hatua ya serikali kuhusu uvaaji wa barakoa ingelianza kutumika Agosti 1, lakini imeharakishwa kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa huo katika baadhi ya maeneo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.