Pata taarifa kuu
UFARANSA-CORONA-AFYA-UCHUMI

Emmanuel Macron ataka uvaaji barakoa uwe lazima katika 'maeneo yote ya umma'

Kama nchini Ubelgiji, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kwamba anataka uvaaji barakoa uwe ni lazima katika maeneo ya umma yaliyofungwa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mahojiano ya runinga na waandishi wa habari wa Ufaransa Lea Salame na Gilles Bouleau huko Paris.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mahojiano ya runinga na waandishi wa habari wa Ufaransa Lea Salame na Gilles Bouleau huko Paris. DENIS CHARLET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya sherehe ya Julai 14, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amesema anaazimia kutoa agizo kwa raia wa Ufaransa kuvaa barakoa katika maeneo ya umaa yaliyofungwa na kufufua uchumi na kulifanyia mabadiliko baraza la mawaziri.

Wakati wa mahojiano yake ya kijadi na waandishi wa habari, mahojiano ambayo yalikua yanasubiriwa kwa hamu na gamu, rais wa Ufaransa amezungumzia masuala kadhaa.

Katika juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19, wakati kuna "ishara kwamba umerudi tena ", Rais wa Ufaransa ametangaza kwamba anataka "uvaaji wa barakoa uwe ni lazima katika maeneo yote ya umma yaliyofungwa". Amesema kuwa hatua hiyo inaweza kuanza kutekelezwa tarehe 1 Agosti.

Kuhusu hatua mpya ya raia kutotembea nchini kote Ufaransa, rais Macron amesema, "Sitaki hali hiyo iwepo hapa nchini," bila, hata hivyo, kuzungumzia hatua zozote ikiwa mlipuko wa pili wa ugonjwa huo utatokea.

Rais Macron pia ametangaza kwamba iwapo mlipuko wa pili wa maambukizi ya virusi vya Corona utatokea, watakuwa tayari kukabilianao nao.

"Tuna hifadhi ya vyakula na vifaa vyote ambavyo ni salama na tuna wataalam wako tayari kukabiliana na mlipuko wa pili iwapo utatokea, " amesema rais Macon.

Kuhusu suala la chanjo dhidi ya Corona, Rais Emmanuel Macron amebaini kwamba itakuwa "ujinga" kuweka mbele "utaifa kwa afya" na kwamba ikiwa chanjo itatengenezwa, Ufaransa itakuwa kati ya nchi za kwanza ambazo zitanufaika na chanjo hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.