Pata taarifa kuu
Gurudumu la Uchumi

Je, ni kweli China inanyonya uchumi wa bara la Afrika kwa kusaini mikataba mikubwa na bara hili

Imechapishwa:

Msikilizaji wa rfikiswahili, hivi karibuni nchi ya China imekuwa mwekezaji mkubwa kwenye sekta za maendeleo na uchumi kwa bara la Afrika, hali ambayo sasa hata mataifa ya magharibi kama vile Marekani imekuwa ikikosoa uwekezaji wa China barani Afrika.

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakishuhudia utiwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa reli toka Nairobi hadi Sudan Kusini.
Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakishuhudia utiwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa reli toka Nairobi hadi Sudan Kusini. Ikulu Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Kwenye makala ya gurudumu la uchumi juma hili, mtangazaji wa makala haya amezungumzia kuhusu uwekezaji huu unaofanywa na China kwa nchi za Afrika hasa kwa kutulianza saini mikataba ya mabilioni ya dola za Marekani kwaajili ya kufadhili miradi ya kimaendeleo.

Wachambuzi wa mambo licha ya kuona kuwa uwekezaji huu ni muhimu, wanaonya kuwa lazima mataifa ya Afrika yawe makini yanapoingia mktaba na nchi ya China kwa kuangalia kwanza nchi zenyewe zitanufaika na nini na uwekezaji huo.

Mfano hivi karibuni, Serikali ya China imetiliana saini mkataba wa dola bilioni 8.2 na viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwaajili ya ujenzi wa reli kutoka Nairobi, Kampala, Kigali, Bujumbura hadi Sudan Kusini ukiwa ni mkataba mkubwa kusainiwa na Serikali ya China.

Lakini je uwekezaji huu wa China unamanufaa yoyote kwa bara la Afrika ama kuna ukweli kwamba wanatumia udhaifu wa bara hili katika kutumia fursa za kiuchumi kujinufaisha?

Mtangazaji wa makala hii amezungumza na Dr. Wetengere Kitojo mtaalamu wa masuala ya uchumi na mhadhiri katika chuo kikuu cha Diplomasia cha jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Vipindi vingine
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.