Pata taarifa kuu

Marekani: Joe Biden apewa shinikizo kuhusu uungwaji mkono kwa Israel

Uungaji mkono wa Joe Biden kwa Israeli unazidi kukosolewa katika kambi ya Democratic. Wakati rais anayemaliza muda wake yuko katikati ya kampeni zake za kuchaguliwa tena. Takriban wabunge 90 jana walitaka kusitishwa kwa uuzaji wa silaha kwa Israel.

Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mnamo Oktoba 18, 2023 huko Tel Aviv.
Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mnamo Oktoba 18, 2023 huko Tel Aviv. via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Katika barua kwa Ikulu ya White House, wajumbe 88 wa Congress wanaeleza "wasiwasi mkubwa" kuhusu mwenendo wa serikali ya Israel katika vita huko Gaza. Suala lililopo ni vikwazo vilivyowekwa na Israel katika upatikanaji wa misaada ya kibinadamu. Misaada iliyotolewa kwa usaidizi wa Marekani, ambayo ina maana ya kufuata sheria za Marekani kuhusu misaada ya kibinadamu nje ya nchi.

Ushahidi

Kwa mujibu wa viongozi hao waliochaguliwa, kuna ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa Israel inakiuka sheria za Marekani: "Kwa hiyo ni lazima tufanye kila kitu ili kumfanya Waziri Mkuu wa Israel aelewe kwamba tabia hii inahatarisha kustahiki kwa nchi yake kupata msaada mpya wa Marekani kwa usalama wake".

Mwezi wa Februari mwaka jana, baada ya wabunge na maseneta wa chama cha Democratic kuondoa kizuizi cha kwanza, Joe Biden alimwagiza Waziri wa Mambo ya Nje kuhakikisha kuwa matumizi ya silaha za Marekani yanafuata sheria za kimataifa.

Tangu wakati huo, angalau ofisi nne za Wizara ya Mambo ya Nje zimemjulisha Antony Blinken kwamba wanabaini uhakikisho wa Israeli wa kutekeleza masharti hayo "si wa kweli wala wa kuaminika." Antony Blinken anatarajiwa kuripoti suala hilo kwa Baraza la Congress kufikia Jumatano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.