Pata taarifa kuu

Vita Gaza: Ujumbe wa Hamas 'utarejea' Cairo na 'jibu' juu ya usitishwaji vita

"Matumaini ya tahadhari kuhusu usitishaji vita huko Gaza" ni hisia ya maafisa wa Misri baada ya majadiliano yao Jumapili Aprili 28 na ujumbe wa Hamas, na siku mbili mapema na maafisa wa Israeli huko Tel Aviv.

Ibada ya fanyika kabla ya mazishi katika makaburi ya Al-Salam, mashariki mwa Rafah, Ukanda wa Gaza, Jumatatu Aprili 29, 2024.
Ibada ya fanyika kabla ya mazishi katika makaburi ya Al-Salam, mashariki mwa Rafah, Ukanda wa Gaza, Jumatatu Aprili 29, 2024. AP - Mohammad Jahjouh
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa Hamas ulitangaza kwamba utarejea Cairo na jibu la mapendekezo ya hivi punde kutoka kwa wapatanishi wa Misri, anaripoti mwandishi wetu huko Cairo, Alexandre Buccianti. Tovuti ya habari ya al-Qahera, iliyo karibu na idara ya ujasusi ya Misri, imebaini kwamba, kwa mujibu wa "vyanzo vya Misri", ujumbe wa Hamas "utarejea na majibu ya maandishi kwa pendekezo la kusitisha mapigano" huko Gaza.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, mafanikio yalipatikana baada ya Israel kulegeza msimamo kuhusu usitishaji vita wa kudumu kufuatia mabadilishano ya mateka wa Israel na wafungwa wa Kipalestina. Sharti linalotakiwa na Hamas.

Kwa hivyo kungekuwa na usitishwaji vita wa takriban siku arobaini na kufuatiwa na mazungumzo ya kusitisha mapigano. Kulianza hata kujadiliwa kwa mustakabali wa mamlaka huko Gaza na ujenzi wake upya wakati wa mkutano wa kiuchumi huko Saudi Arabia ambao ulileta pamoja mkuu wa diplomasia ya Marekanii na wenzake wa Kiarabu.

Shinikizo la Waarabu

Lakini shetani yuko katika maelezo, tunangoja majibu ya Hamas huku tukitoa shinikizo la busara kwa upande wa nchi za Kiarabu. Suala la uwezekano wa Qatar kuondoka katika uongozi wa kisiasa wa jumuiya ya Kiislamu liliibuliwa katika mahojiano Jumapili na afisa mkuu wa Hamas, ingawa aliongeza kuwa "hili halikuwepo mezani." Zaher Jabareen, mmoja wa wapatanishi wa Hamas, pia ameliambia shirika la habari la AFP kwamba "ni mapema mno kuzungumza juu ya hali nzuri katika mazungumzo". Mbali na usitishaji vita wa kudumu, Hamas pia inadai "kuondoka kwa  Israeli kutoka Ukanda wa Gaza, kurejeshwa kwa waliokimbia makazi yao, ratiba ya wazi ya kuanza kwa ujenzi mpya na makubaliano ya kubadilishana mateka wa Israel na wafungwa wa kipalestin, hali ambayo itaondoa dhuluma yoyote kwa wafungwa wa Kipalestina, wanaume na wanawake,” amesema.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, baraza la mawaziri la vita la Israel hapo awali lilidai kuachiliwa kwa mateka 40 waliokuwa wameshikiliwa huko Gaza, kabla ya kuwaruhusu wafanya mazungumzo kupunguza idadi hiyo. Tovuti ya habari ya Marekani ya Axios ilionyesha kuwa Israel ilikuwa inadai kuachiliwa kwa wanawake, raia au wanajeshi, na wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 50 au wenye afya mbaya. Kulingana na Axios, Hamas inadai kuwa ni mateka 20 pekee wanaokidhi vigezo hivi. Tovuti hiyo inaongeza kuwa idadi ya siku za usitishwaji vita itakuwa sawa na ile ya mateka watakaoachiliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.