Pata taarifa kuu

UN yazungumzia uwezekano wa 'uhalifu wa kivita' baada ya mashambulizi ya Israel

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema "amechukizwa" na mashambulizi ya angaa kwenye kambi ya Jabaliya katika Ukanda wa Gaza, ambako wakimbizi 116,000 wanaishi.

Wanajeshi wa jeshi la Israeli wakipiga kambi katika eneo la kaskazini mwa Galilaya mnamo Novemba 1, 2023, kwenye mpaka kati ya Lebanon na Israeli, ambapo mapigano ya kila siku huripotiwa.
Wanajeshi wa jeshi la Israeli wakipiga kambi katika eneo la kaskazini mwa Galilaya mnamo Novemba 1, 2023, kwenye mpaka kati ya Lebanon na Israeli, ambapo mapigano ya kila siku huripotiwa. © JALAA MAREY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano jioni Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu alibaini kwamba milipuko hii inaweza kujumuisha "uhalifu wa kivita", "kulingana na idadi kubwa ya waathiriwa wa kiraia na ukubwa wa uharibifu".

Mkuu wa kitengo cha jeshi la Hamas auawa

Waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP waliweza kuona uharibifu mkubwa katika eneo la tukio, ambapo manusura walikuwa wakipita kwenye vifusi kutafuta wenzao. Waokoaji wamesema "familia nzima" zimeangamia katika mashambulizi hayo.

Jeshi la Israel, ambalo linaendelea na mashambulizi makali huko Gaza kujibu mashambulizi ya umwagaji damu ya Hamas mnamo Oktoba 7, limedai kumuua mkuu wa kitengo cha jeshi la Hamas, Muhammad Atzar, katika mashambulizi yake kwenye kambi ya Palestina siku ya Jumatano.

Operesheni ya kwanza ya kuwahamisha watu siku ya Jumatano iliwawezesha Wapalestina 76 waliojeruhiwa na wageni 335 na raia wenye uraia pacha, kulingana na afisa wa Misri, kuondoka katika eneo hilo kupitia kituo cha mpaka cha Rafah, pekee ambacho hakijadhibitiwa na vikosi vya Israeli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.