Pata taarifa kuu

Gaza: Jeshi la Israel latangaza vifo vya wanajeshi wake wawili katika mapigano

Jeshi la Israel limetangaza siku ya Jumanne kuwa wanajeshi wake wawili wameuawa katika mapigano kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, katika siku ya 25 ya vita dhidi ya kundi la Hamas.

Mwanajeshi wa Israel akipiga doria kando ya uzio kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza, Oktoba 25, 2023.
Mwanajeshi wa Israel akipiga doria kando ya uzio kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza, Oktoba 25, 2023. AFP - ARIS MESSINIS
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao wawili "wameangamia katika mapigano kaskazini mwa Ukanda wa Gaza," jeshi limesema katika taarifa, saa chache baada ya kuripoti "mapigano makali" na Hamas katika eneo hilo.

Katika ukurasa wa Wizara ya Ulinzi, majina ya askari 317 "wahanga wa vita" yanaonyeshwa. Majina mawili ya mwisho kwenye orodha: Sajenti Levi Lifshitz, anayefanya kazi kwa idara ya upelelezi. Mwingine, Sajini Roy Wolf. Wote wawili wameuawa mnamo Oktoba 31.

Mashambulizi ya ardhini

Jeshi la Israel linaongeza mashambulizi yake ya ardhini huko Gaza baada ya kutekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya kambi kwa siku kadhaa. Uvamizi wa ndani ulifanyika kwanza, hapo awali kwa kutumia magari ya kivita.

Israel inasema "inaendelea kwa utaratibu, hatua kwa hatua" katika eneo hilo na inaamini kwamba mashambulizi makubwa ya kijeshi ya ardhini bado hayajaanza.

Siku ya Jumatatu Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alifutilia mbali usitishaji vita wowote ambao alisema itakuwa "kujisalimisha kwa Hamas". Marekani inashiriki msimamo huu, ikiamini kwamba mapatano hayo yanaweza kunufaisha kundi hilo la kigaidi lenye silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.