Pata taarifa kuu

Uchambuzi: Iran kwenye kizingiti cha matamanio yake ya nyuklia

Tehran imepiga tena hatua katika maendeleo ya mpango wake wa nyuklia: Jamhuri ya Kiislamu sasa inarutubisha uranium hadi 60% katika eneo la pili, lile la Fordo. Kuongezeka huko kwa kasi kunakuja kwani hakuna mazungumzo tena ya makubaliano mapya ya nyuklia. Na wakati Iran inazidi kutengwa kutokana na ukandamizaji wa maandamano ambayo yamekuwa yakiendelea tangu mwezi Septemba.

Mwonekano wa angani wa satellite wa kiwanda cha mafuta cha Fordo mnamo 2020.
Mwonekano wa angani wa satellite wa kiwanda cha mafuta cha Fordo mnamo 2020. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Agosti 2022, kulikuepo na matumaini huko Vienna, mji mkuu wa Austria. Vyanzo vingi vilitabiri kufufuliwa kwa makubaliano ya nyuklia (JCPOA, ilifikiwa mnamo 2015 na kisha kudhoofishwa na kujiondoa kwa Marekani bada ya kuagizwa na  Donald Trump mnamo 2018). Lakini majira ya joto yalimalizika na mazungumzo ya Vienna yalirejelewa bila matokeo "kwa sababu ya msimamo usio na maana wa Iran", kulingana na Robert Malley, mjumbe maalum wa rais wa Marekani kwa Iran, ambaye RFI ilikutana naye mwanzoni mwa mwezi wa Novemba wakati wa ziara yake mjini Paris.

"Tulikuwa karibu sana na makubaliano lakini katika dakika ya mwisho, Iran iliamua kurejesha matakwa yasiyoeleweka na yasiyokubalika", alieleza Robert Malley ambaye aliongeza kuwa mazungumzo pia yalibadilika: Iran inatikiswa na maandamano ambayo hayajawahi kutokea na ndege zisizo na rubani za Iran kulipuka katika anga ya Ukraine ikisaidia jeshi la Urusi.

Hakuna mazungumzo yanayotarajiwa, lakini Iran inaendelea kupiga hatua katika mpango wake na ilitangaza mnamo Novemba 22 kwamba imeanza kurutubisha uranium hadi 60% katika eneo la Fordo. Mwaka jana, Iran tayari ilikuwa imefikia kiwango hiki cha urutubishaji katika eneo la Natanz, wakati makubaliano ya nyuklia ya 2015 (Joint Comprehensive Plan Of Action, JCPOA) yanaweka kikomo cha kurutubisha uranium hadi 3 .67%, kiwango kinachoendana na mpango wa nyuklia wa kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.