Pata taarifa kuu

Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa lafungua uchunguzi kuhusu ukandamizaji Iran

Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi limeanzisha uchunguzi wa kimataifa kuhusu ukandamizaji wa umwagaji damu dhidi ya maandamano yanayoendelea nchini Iran, ili kukusanya ushahidi unaowezekana kuwafungulia mashtaka waliohusika.

Picha za wahanga waliouawa na utawala wa Iran mbele ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakati wa kikao maalum cha Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Iran.
Picha za wahanga waliouawa na utawala wa Iran mbele ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakati wa kikao maalum cha Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Iran. © AFP - VALENTIN FLAURAUD
Matangazo ya kibiashara

Azimio lililowasilishwa na Ujerumani na Iceland limepitishwa kwa kura 25 za "ndiyo", kura sita za "hapana" na kura kumi na sita ambazo hazikutoa msimamo wowote katika mkutano wa dharura wa Baraza la Haki za Kibinadamu huko Geneva.

Mkutano huo ulioombwa na Ujerumani na Iceland na kuungwa mkono na zaidi ya nchi 50, unafuatia miezi miwili ya maandamano nchini Iran yaliyochochewa na kifo cha Mahsa Amini msichana wa kikurdi mwenye umri wa miaka 22. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amelitaka baraza hilo "kupaza sauti" kuhusu ukandamizaji mbaya dhidi ya waandamanaji nchini Iran. 

Kwa mujibu wa kundi la kutetea Haki za Kibinadamu la Iran lenye makao yake nchini Norway, zaidi ya watu 400 wameuawa kote nchini Iran, wakati wa ukandamizaji kwenye vurugu za maandamano. Umoja wa Mataifa unasema maelfu ya waandamanaji wa amani wakiwemo wanawake, watoto na waandishi wa habari pia wamekamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.