Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

Picha ya mwaka wa 1994 inasambazwa nchini DRC kudai ni ya sasa

Imechapishwa:

Sasa kuna picha ambayo insambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuoyesha mtoto akilia huku akionekana kumvuta na kumkwamilia mwanamume aliyelala chini ikiwa imeambatanishwa na madai kwamba inaonyesha "mauaji ya kimbari" yanayoendelea kwa sasa nchini DRC.

Picha ya zamani inayosambaa nchini DRC ikidai kumuonyesha mtoto aliye kando ya baba yake aliyeuawa na waasi
Picha ya zamani inayosambaa nchini DRC ikidai kumuonyesha mtoto aliye kando ya baba yake aliyeuawa na waasi © fmm
Matangazo ya kibiashara

Lakini muktadha wa chapisho hilo ni wa kupotosha: Japokuwa picha yenyewe ilitokea na ni ya kweli, ilipigwa mwaka wa 1994 na inaonyesha mvulana mwenye asili ya Rwanda karibu na baba yake ambaye alifariki baada ya kuambukizwa kipindupindu nchini DRC.

Kwa mujibu wa maelezo kwenye makataba ya Getty images, yanaoonyesha mtoto raia wa Rwanda akilia huku akimng'ang'ania baba yake aliyefariki kutokana na  ugonjwa wa kipindupindu mwaka 1994 huko Zaire, ambayo sasa inajulikana kama DRC.

Wawili hao walikuwa wamekimbia ghasia kati ya Wahutu na Watutsi nchini Rwanda na kuja nchini Zaire kwa ajili ya usalama wao, kwa mujibu wa maelezo kwenye picha hiyo.

Vipindi vingine
  • 09:57
  • 10:02
  • 10:18
  • 10:00
  • 10:00
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.