Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

Habari za kupotosha kuhusu virusi vya HIV na tembe za kupunguza makali

Imechapishwa:

Hujambo na karibu katika kipindi hiki cha UKWELI au UONGO kutoka RFI Kiswahili. Hapa mskilizaji tunaangazia jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii ili kukuepuka habari za Uongo

Fake news claiming that if one uses painkillers before going for a HIV test they will be found negative of the virus.
Fake news claiming that if one uses painkillers before going for a HIV test they will be found negative of the virus. © FMM-RFI
Matangazo ya kibiashara

Tuangazie taarifa kwenye mtandao wa TikTok, iliyosambaa sana mwishoni mwa mwezi Februari, video hii ilikuwa na madai ya kushangaza.

Mtumiaji wa huu mtandao aliyetumia mchanganyiko wa lugha ya Kingereza na Kiswahili, ambayo inazungumzwa sana miji mingi nchini Kenya, anadai kugundua siri kuwa iwapo mtu ana virusi vya HIV, na akunywe dawa ya kupunguza maumivu, basi akipimwa atakuwa hana virusi hivyo.

Video hii iliwapotosha watu wengi sana, maana ilitazamwa na zaidi ya watu milioni 1.6, ikiwa na maoni zaidi ya elfu sita na ilisambazwa zaidi ya mara elfu tisa.

Wataalama wa afya wamethibitisha taarifa hii kuwa ya kupotosha na ya uongo.

Vipindi vingine
  • 09:57
  • 10:02
  • 10:18
  • 10:00
  • 10:00
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.