Matumizi ya dawa za kulevya ,umeendelea kuwa mzigo katika mataifa mengi ,familia nyingi zikilazimika kuwapoteza jamaa zao ambao wangechangia ujenzi wa taifa
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani ,WHO ,kuna watu karibu milioni 40 ambao wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya na wanaohitaji msaada wa matibabu ya kitalaam kuwarejesha katika hali zao za kawaida.
Kwenye makala haya tumezungumza na raia,watu waliotumia dawa za kulevya ,walio wahi kuuza na watalaam kuhusu swala zima la dawa za kulevya. Je ina manufaa yoyote?