Habari RFI-Ki
Serikali ya Uingereza yatangaza fidia ya £19.9 milioni kuwalipa waathirika wa Vita Vya Mau Mau nchini Kenya
Imechapishwa:
Cheza - 10:12
Wapiganaji wa Vita vya Mau Mau nchini Kenya vilivyokwenda sanjari na harakati za kudai Uhuru nchini Kenya wapatao 5,228 hatimaye wamelipwa fidia yenye thamani ya £19.9 milioni kutoka Serikali ya Uingereza kutokana na unyanyasi na mateso waliyokumbana nayo zaidi ya miaka 50 yaliyopita. Wapiganaji hao wa Mau Mau wamepata fidia yenye thamani ya £2600 kwa kila mmoja kutokana na kushinda kesi yao iliyokuwa inasikilizwa nchini Uingereza!!