Pata taarifa kuu
KENYA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Kenya yaendelea kutangaza maambukizi zaidi

Wizara ya afya nchini Kenya imesema watu wengine 11 wamepatikana na virusivya Corona katika jiji kuu Nairobi na mji wa Pwani wa Mombasa kwa saa 24 zilizopita na kufikisha idadi ya watu walioambukizwa kufikia 374, huku wengine 10 wakipona na kufikisha idadi ya watu waliopona kufikia 124.

Wakazi wa Kibera jijini Nairobi wanarudi nyumbani kabla ya amri ya kutotoka nje kutekelezwa katika mapambano dhidi ya Corona Machi 27, 2020.
Wakazi wa Kibera jijini Nairobi wanarudi nyumbani kabla ya amri ya kutotoka nje kutekelezwa katika mapambano dhidi ya Corona Machi 27, 2020. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Mapma wiki hii serikali ya Kenya ilitangaza kuanza kufunguliwa tena kwa hoteli na Migahawa kipindi hiki nchi hiyo inapoendela kukabiliwa na janga la Corona.

Wizara ya afya ilitoa agizo la watu wote wanaoingia migahawani kupimwa kiwango cha joto na kuruhusiwa tu kuingia ikiwa kitakuwa chini ya nyuzi 37.5 na mgahawa husika kuarifu wizara mara moja kuhusu mtu atakayepatikana akiwa na kiwango ha juu zaidi ya hicho, kwa kupiga simu kupitia nambari 719 ili kupata mwongozo zaidi.

Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe alisema kuwa biashara itaruhisiwa tu kati ya saa 11 asubuhi hadi saa 10 jioni.

Katika kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19, serikali imeunda kamati 5 za kimkakati kutoa mwongozi wa njia zitakazofanikisha kenya kushinda vita hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.