Pata taarifa kuu
KENYA-CORONA-AFYA

Idadi ya maambukizi yafikia 320 Kenya

Watu wengine 17 wamepatikana na virusi vya Corona nchini Kenya na kufikisha idade ya walioambukizwa kufikia 320, wakati huu ikiripotiwa kuwa maambukizi yanaongezeka sana mjini Mombasa hasa kati ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari.

Ugonjwa wa Covid-19 unaendelea kuiathiri Kenya.
Ugonjwa wa Covid-19 unaendelea kuiathiri Kenya. REUTERS/Njeri Mwangi
Matangazo ya kibiashara

Katibu wa kudumu katika Wizara ya Afya Dkt. Mercy Mwangangi amesema kwamba wagonjwa 15 kati yao walipatikana kupitia uchunguzi wa serikali, huku wawili wakiwa katika vituo vya karantini.

Hata hivyo amsema kwamba wamegundua kwamba wakazi wa Mombasa wamekuwa wakiambukizana wenyewe kwa wenyewe.

Wizaya hiyo imetangaza kwamba wagonjwa wote ni raia wa Kenya, huku iripoti idadi ya waliopona nchini humo kuwa watu 89 baada ya wagonjwa sita zaidi kuwachiliwa baada ya kuripotiwa kupona virusi hivyo.

Kwa siku ya nne mfululizo Mombasa imeongoza kwa idadi ya wagonjwa wapya wa Covid 19 nchini Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.