Pata taarifa kuu
EAC

Wana-Afrika Mashariki watakiwa kuufahamu wimbo wa Jumuiya

Idara mbalimbali za serikali katika Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, zimeanza kutekeleza maelekezo ya serikali zao kuanza kupeperusha Bendera ya Jumuiya hiyo sambamba na ile ya taifa katika Ofisi zao.

Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC
Matangazo ya kibiashara

Mbali na Bendera, wimbo wa Jumuiya hiyo umetakiwa kuimbwa katika shughuli zote za kitaifa, pindi tu baada ya ule wa taifa husika.

Jumuiya ya Afrika Mashariki ina mataifa matano; Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini ambayo ilijiunga mwaka huu.

Bendera na wimbo wa taifa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni nembo muhimu zinazoonesha umoja wa watu wa Afrika Mashariki kuelekea kwenye shirikisho la kisiasa katika siku zijazo.

Mwisho wa mwezi uliopita, serikali ya Kenya iliagiza bendera ya Jumuiya kupeperushwa sambamba na ile ye taifa na wimbo wa Jumuiya kuchezwa katika shughuli zote za kitaifa.

Agizo kama hili lilitolewa nchini Tanzania na limeanza kutekelezwa sawa na Uganda ambayo imekuwa katika mstari wa mbele kutekeleza hili kwa muda mrefu sasa.

Nembo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Nembo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC

Wana Afrika Mashariki wamekuwa wakihimizwa kuufahamu wimbo wa Jumuiya;

WIMBO WA JUMUIYA

Kiitikio
Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.
 

Stanza
1.Ee Mungu twaomba ulinde
Jumuiya Afrika Mashariki
Tuwezeshe kuishi kwa amani
Tutimize na malengo yetu.

2.Uzalendo pia mshikamano
Viwe msingi wa Umoja wetu
Natulinde Uhuru na Amani
Mila zetu na desturi zetu.

3.Viwandani na hata mashambani
Tufanye kazi sote kwa makini
Tujitoe kwa hali na mali
Tuijenge Jumuiya bora.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.