Pata taarifa kuu

Mpango wa Uingereza kutuma waomba hifadhi Rwanda umepata pigo jingine

Nairobi – Mpango wa Serikali ya Uingereza, kuwatuma waomba hifadhi nchini Rwanda, umepata pigo jingine baada ya bunge la wawakilishi kupiga kura kurejesha mapendekezo yao ya awali, ambayo yalikataliwa na bunge.

Watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakipinga huo wakisema kuwa ni kinuyme na sheria.
Watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakipinga huo wakisema kuwa ni kinuyme na sheria. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa wawakilishi, unaonesha kile wadadisi wa siasa za Uingereza, wamesema mgawanyiko mkubwa kuhusu muswada wa usalama wa nchi ya Rwanda, ambao waziri mkuu Rishi Sunak na Serikali yake wamekuwa wakiupigia chapuo.

Kwa watetezi wa haki za binadamu, wanaunga mkono uamuzi wa wawakilishi licha ya kuwa mapendekezo yao ya awali yalikataliwa yote na wabunge wa kitaifa, sasa muswada huo ukitarajiwa kujadiliwa na mabunge yote mawili kabla ya kuamuliwa.

Miongoni mwa vipengele vinavyopingwa ni pamoja na kuitaja Rwanda kama nchi salama kwa wahaliaji na kuzuia mahakama za ndani na nje kutokuwa na uwezo wa kuzuia mpango huo kisheria.

Rwanda imeendelea kusisitiza kuwa ni nchi salama kwa wakimbizi licha ya watetezi wa haki za binadamu kupinga mpango huo wa kutumwa kwa waomba hifadhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.