Pata taarifa kuu

Kenya: Hospitali za umma zakumbwa na mgomo wa madaktari

Baadhi ya hospitali za umma zimeshuhudia shughuli zao zikipungua siku ya Alhamisi nchini Kenya, zaidi ya wiki moja baada ya kuanza kwa mgomo wa kitaifa wa madaktari wakitaka mazingira bora ya kazi na nyongeza ya mishahara.

Watu waliojeruhiwa wakitembea kutafuta kivuli baada ya kutibiwa katika Hospitali ya Mama Lucy Kibaki kutokana na majeraha waliyopata kufuatia mlipuko wa gesi eneo la Embakasi Nairobi, Februari 2, 2024.
Watu waliojeruhiwa wakitembea kutafuta kivuli baada ya kutibiwa katika Hospitali ya Mama Lucy Kibaki kutokana na majeraha waliyopata kufuatia mlipuko wa gesi eneo la Embakasi Nairobi, Februari 2, 2024. Β© Tony KARUMBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini Kenya (KMPDU), pekee katika sekta ya matibabu yenye wanachama zaidi ya 7,000, ulizindua maandamano haya mnamo Machi 13. "Serikali haijaonyesha nia ya kuondokana katika hali hii," naibu katibu mkuu wa KMPDU Dennis Miskellah ameliambia shirika la habari la AFP.

"Hatutarejea kazini hadi matakwa yetu yatimizwe," amesema. Ili kukabiliana na mgomo huo, hospitali zilizoathiriwa zimetoa wito kwa wauguzi na matabibu, ambao hata hivyo wana upungufu wa huduma wanazoweza kutoa.

Wiki jana mahakama iliamuru kusitishwa kwa mgomo huo na kutaka mazungumzo yafanyike, lakini KMPDU ilitangaza kwamba itaendeleza hatua yake. Madaktari hao waliohamasishwa wanapinga hasa uamuzi wa serikali unaolenga kupunguza mishahara ya wahudumu wa afya na kurudisha nyuma umri wa kustahiki haki za kustaafu.

Madaktari hao wamepanga kuandamana siku ya Ijumaa kwa kwenda kwa Wizara ya Afya na majengo kadhaa ya serikali katika mji mkuu Nairobi, kama vile bunge na kwenye makao makuu ya Hazina ya umma. Serikali ilitishia kuajiri madaktari wasio na kazi kuchukua nafasi za waliogoma.

"Hatutaruhusu mgogoro kutokea," Waziri wa Afya Susan Nakhumicha aliambia runinga ya KTN siku ya Jumatano, akiongeza kwamba aliomba hospitali kuu mbili kuajiri watu wengine ili kufidia uhaba huo. "Tuna wagonjwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi, ... tuna watoto katika vitengo vya watoto wachanga," alingeza.

Katibu Mkuu wa KMPDU amelaani "vitisho" vya waziri. "Wanapotoa vitisho zaidi, ndivyo mgomo utakavyokuwa mrefu," Davji Atellah ameliiambia shirika la habari la AFP. Mnamo mwaka wa 2017, chama hiki kilianzisha mgomo katika nchi hii ya Afrika Mashariki, ambao ulidumu karibu siku mia moja, kiikitaka nyongeza kubwa ya mishahara na mazingira bora ya kazi, ikijumuisha vifaa bora katika hospitali za umma.

Madaktari wanaogoma bado wanashutumu serikali leo kwa kutotimiza baadhi ya ahadi zilizotolewa katika makubaliano ambayo yalifuatia maandamano haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.