Pata taarifa kuu

Uingereza: Mpango wa kuwatuma waomba hifadhi nchini Rwanda umepiga hatua

Nairobi – Mpango wa waziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak, kuwatuma wanaotafuta hifadhi nchini Rwanda umepiga hatua katika bunge, baada ya watunga sheria hao kupiga kura kutupilia mbali msururu wa marekebisho yaliyofanywa kwenye mswada huo na bunge la wawakilishi.

Miongoni mwa maboresho yaliyopendekezwa ni pamoja na nchi hiyo kuheshimu sheria za kimataifa.
Miongoni mwa maboresho yaliyopendekezwa ni pamoja na nchi hiyo kuheshimu sheria za kimataifa. © Daniel Leal / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wabunge walipiga kura kuyakataa marekebisho yote 10 yaliyofanywa na wenzao wiki chache zilizopita, uamuzi huu ukionakana kama ushindi kwa Sunak, ambaye anaharakisha muswada huo kupitishwa.

Muswada kuhusu usalama wa nchi ya Rwanda, ambao umetengenezwa ili kuzuia mahakama yoyote kuingilia uamuzi wa Serikali, utarejeshwa tena katika bunge la wawakilishi wiki hii, ambapo litaamua ikiwa liunge mkono au liucheleweshe zaidi.

Watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakipinga mpango huo wakisema unakiuka haki za binadamu.
Watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakipinga mpango huo wakisema unakiuka haki za binadamu. © Getty Images

Kukataliwa kwa marekebisho hayo kunatoa afueni kwa waziri mkuu, ambaye kwa miezi sasa amekuwa akiwataka wabunge kuunga mkono kwa kile anasema utasaidia pakubwa kuzuia wimbi la waomba hifadhi licha ya kukosolewa na watetezi wa haki za binadamu.

Miongoni mwa maboresho yaliyopendekezwa ni pamoja na nchi hiyo kuheshimu sheria za kimataifa, na kutoitangaza Rwanda kama nchi salama hadi pale tathmini ya kina itakapofanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.