Pata taarifa kuu

Uingereza: Serikali yapata pigo kuhusu muswada wa kupeleka wahamiaji Rwanda

Nairobi – Waziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak, amepata pigo la kwanza kuhusu muswada wake tata wa kupeleka wahamiaji nchini Rwanda, baada ya bunge la wataalamu kuitaka serikali kuweka sheria zitakazowalinda wahamiaji hao.

Chini ya mpango huu ambao bado haujaanza kutekelezwa, waomba hifadhi wanaowasili nchini humo, watatumwa kuishi nchini Rwanda
Chini ya mpango huu ambao bado haujaanza kutekelezwa, waomba hifadhi wanaowasili nchini humo, watatumwa kuishi nchini Rwanda AFP - GLYN KIRK
Matangazo ya kibiashara

Chini ya mpango huu ambao bado haujaanza kutekelezwa, waomba hifadhi wanaowasili nchini humo, watatumwa kuishi nchini Rwanda, wakati wakisubiri uamuzi wa mchakato wa maombi yao.

Awali waziri mkuu Rishi Sunak, alitumia bunge la kitaifa ambako anauungwaji mkono kupitisha muswada huu ambao unakataza makahama yoyote kuzuia kutekelezwa kwake.

Uamuzi wa baraza hili la wabunge wasiochaguliwa, unamaanisha kuwa Serikali italazimika kupitia upya mapendekezo yaliyotolewa kabla ya kuanza kuutekeleza.

Bunge hili linaloundwa na wanasiasa wa zamani na wafanyakazi wa uma, pia walitaka ushahidi kuwa Rwanda ni nchi salama na pia muswada huo lazima uzingatie sharia za ndani na zile za kimataifa, hata hivyo bunge la House of Commons loinaweza kubatilisha uamuzi wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.