Pata taarifa kuu

Tanzania inataka kurudisha wakimbizi waliopo kwenye ardhi yake katika nchi yao ya asili

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alitangaza siku ya Jumatatu Januari 22 nia yake ya kuwarejesha zaidi ya wakimbizi 200,000 waliopo katika ardhi ya Tanzania katika nchi yao ya asili. Hii ikirasimishwa, wakimbizi hawa wataondoka nchini Tanzania kwa hiari, shinikizo juu yao linaongezeka.

Wakimbizi wa Burundi katika kambi ya wakimbizi ya Nduta mkoani Kigoma kaskazini magharibi mwa Tanzania, Oktoba 2015.
Wakimbizi wa Burundi katika kambi ya wakimbizi ya Nduta mkoani Kigoma kaskazini magharibi mwa Tanzania, Oktoba 2015. AFP Photo/Oxfam/Mary Mndeme
Matangazo ya kibiashara

 

Samia Suluhu Hassan alieleza nia yake ya kuwarudisha makwao wakimbizi wote walio katika ardhi ya Tanzania siku mbili zilizopita jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano na kamanda mkuu wa TDF, jeshi la Tanzania, ambaye alimuuliza. "Kama mkuu wa nchi, nimezingatia pendekezo lako la kuwatambua wakimbizi wote wanaoishi Tanzania, (...) ili tuone jinsi ya kuwarudisha katika nchi yao ya asili," alisema Rais wa Tanzania.

 

Mnamo Juni 2023, kwa mujibu wa takwimu za Tume Kuu ya Umoja wa Mataifa (UNHCR), nchi hiyo inawahifadhi zaidi ya wakimbizi 250,000, theluthi mbili kati yao wameitoroka Burundi tangu mgogoro wa 2015. Wengine wengi ni wakimbizi wa Kongo wanaotoka mashariki mwa DRC, inayokumbwa na ghasia za mara kwa mara za kutumia silaha.

 

Kwa miaka kadhaa, Tanzania imekuwa ikizingatia kwamba wakimbizi hawa ni mzigo unaoongezeka wa kiuchumi na wanaweza kuwa tishio la usalama: kwa hiyo inataka kuwaona wakiondoka. Lakini kampeni zote zilizowekwa kwa nia ya kurejea kwa hiari au vikwazo vya kila aina hazijafaulu kuwashawishi wakimbizi, hasa Warundi, kurejea kwa wingi katika nchi yao ya asili.

 

Hata kama Samia Suluhu anaishutumu UNHCR kwa kutotekeleza misheni yake, aliahidi jeshi lake Jumatatu Januari 22 kuendelea "kufanya kazi" na shirika la Umoja wa Mataifa. Anategemea zaidi ya yote "mazungumzo ya kisiasa" na nchi zinazohusika, anasema, kutatua suala hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.