Pata taarifa kuu

Kigali yakashifu matamshi ya Bujumbura dhidi yake

Nairobi – Serikali ya Rwanda kupitia taarifa kwenye mtandao wa X, imekashifu matamshi yaliotolewa na rais wa Burundi Evariste Ndayishimye wikendi iliopita akiwa jijini kinshasa nchini DRC, ambayo inasema yalilenga kuchochea mgawanyiko miongoni mwa vijana raia wa Rwanda na kuhatarisha amani na usalama katika ukanda wa maziwa makuu.

Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Rwanda Paul Kagame. REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa ya Kigali, raia  wa Rwanda wanafanya bidi kuimarisha umoja na maendeleo na kwamba kwa mtu yeyote kujaribu kuwataka vijana wa taifa hilo kupindua serikali yao ni jambo la kukera.

Aidha Kigali imeeleza kuwa ilikuwa makosa kwa kwa kiongozi wa nchi jirani kutoa matamshi kama hayo katika hafla ya umoja wa Afrika suala ambalo ni ukiukaji wa mkataba wa Umoja huo.

Vilevile utawala wa Kigali umeeleza kuwa hauna haja ya kuzua ghasia na majirani zake na kwamba Rwanda itaendelea kushirikiana na mataifa jirani katika eneo hili na kwengineko kuimarisha udhibiti na maendeleo.

Kwa upande wake, serikali ya Rwanda imeendelea kusema haina uhusiano wowote na kinachoendelea katika nchi jirani zake
Kwa upande wake, serikali ya Rwanda imeendelea kusema haina uhusiano wowote na kinachoendelea katika nchi jirani zake REUTERS - JEAN BIZIMANA

Katika mahojiano na vijana siku ya Jumapili mjini Kinshasa, rais Ndayishimiye alikosoa mamlaka ya Rwanda kwa kusaidia kile ambacho alitaja kuwa makundi yanayovuruga eneo hilo.

Aidha rais Ndayishimiye alisema kuwa ilikuwa muhimu kuendeleza mapambano hadi raia wa Rwanda wenyewe waanze kutoa shinikizo ambapo aliongeza kuwa anadhani hata vijana wa Rwanda hawawezi kukubali kuwa wafungwa katika eneo hilo.

Rais wa Burundi amekuwa akisisitiza kuwa hakuna ukandamizaji wa haki za binadamu nchini mwake.
Rais wa Burundi amekuwa akisisitiza kuwa hakuna ukandamizaji wa haki za binadamu nchini mwake. AFP - TCHANDROU NITANGA

Tangu mwaka uliopita, uhusiano kati ya Bujumbura na Kigali umekuwa ukiyumba baada Burundi kuituhumu Rwanda kwa kusaidia kundi la RED-Tabara lililofanya shambulio baya kaskazini na magharibi mwa nchi yake.

Kwa upande wake, serikali ya Rwanda imeendelea kusema haina uhusiano wowote na shambulio hilo.

Tayari Burundi imetangaza kufunga mpaka wake na jirani yake Rwanda hatua inayokuja wakati huu mzozo kati ya mataifa hayo ukionekana kuongezeka.

Burundi imefunga mpaka wake na Rwanda
Burundi imefunga mpaka wake na Rwanda STEPHANIE AGLIETTI / AFP
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.