Pata taarifa kuu

Tanzania yalaumu ukame kusababisha mgao wa umeme

Nairobi – Shirika la umeme nchini Tanzania, TANESCO, linasema ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na masuala mengine, yamesababisha mgao wa umeme nchini humo. 

Changamoto hiyo inatarajiwa kumalizika baada ya  ujenzi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere kukamilika
Changamoto hiyo inatarajiwa kumalizika baada ya ujenzi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere kukamilika © Statehouse Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia wiki iliyopita, Shirika hilo lilitangaza mpango wa kuanza kusambaza umeme kwa mgao nchi nzima, hali ambayo inaelezwa itaendelea hadi mwezi Machi, mwaka ujao. 

Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Gissima Nyamo-Hanga, amethibitisha hilo, akisema ifikapo mapema mwaka 2024, changamoto hiyo itakuwa imepewa ufumbuzi. 

Aidha, amesema gridi ya taifa inakabiliwa na uharibifu wa miundombinu katika vituo vya umeme vinavyotumia gesi na kupungua kwa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme.  

Hata hivyo, Tanzania inatumai kumaliza changamoto ya mgao wa umeme baada ya kumalizika kwa ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere, linalotarajiwa kuzalisha megawati 2,115 ya umeme. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.