Pata taarifa kuu

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Godbless Lema arejea kutoka uhamishoni

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Godbless Lema amerejea nyumbani Jumatano baada ya kukaa uhamishoni kwa miaka miwili, akilakiwa na wafuasi wake, katika nchi hii ya Afrika Mashariki ambayo imezidisha dalili za uwazi katika miezi ya hivi karibuni, chama chake kimetangaza.

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Godbless Lema, aliyekimbilia nchini Kenya, akijiandaa kuondoka nchini humo kuelekea Canada (09/12/2020)
Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Godbless Lema, aliyekimbilia nchini Kenya, akijiandaa kuondoka nchini humo kuelekea Canada (09/12/2020) COURTESY
Matangazo ya kibiashara

Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema alitorokea nchi ya Tanzania kuelekea Canada Novemba 2020, akibaini kufanyiwa vitisho na mamlaka. Bw. Lema, 46, "amewasili leo mchana (Jumatano) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro", takriban kilomita 70 kaskazini mwa Arusha, chama cha CHADEMA ikimetangaza kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Wafuasi walimkaribisha kwa bendera za rangi ya bluu, nyeupe, na nyekundu, bendera ya chama cha CHADEMA. Mkosoaji wa serikali, Godbless Lema alikuwa amechaguliwa kuwa mbunge kwa miaka 10 kabla ya kupoteza kiti chake mwaka 2020.

Matokeo haya na yale ya uchaguzi wa urais ambayo yalimfanya John Magufuli aliyemaliza muda wake kuchaguliwa tena kwa asilimia 84 ya kura, yalipingwa na upinzani ambao uliitisha maandamano. Lakini viongozi wao walikamatwa haraka. Godbless Lema kisha akakimbilia Kenya pamoja na mkewe na watoto wake kabla ya kupata hifadhi ya kisiasa nchini Canada.

Kurejea kwa Bw.Lema kumekuja ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya kurejea kwa Tundu Lissu, kiongozi wa upinzani na aliyekuwa mgombea urais, ambaye alikaa uhamishoni nchini Ubelgiji kwa takribani miaka mitano baada ya jaribio la kutaka kumuua. Katikati ya mwezi Januari, Rais Samia Suluhu Hassan alitangaza kuondolewa kwa marufuku ya mikutano ya upinzani wa kisiasa.

Marufuku hii ilitangazwa mwaka 2016 na kiongozi wa kimabavu John Magufuli, ambaye alifariki dunia ghafla Machi 2021. Chini ya uongozi wa John Magufuli, aliyepewa jina la utani la "Bulldozer", aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza 2015, mikutano ya kisiasa ilipigwa marufuku, viongozi wa kisiasa wa upinzani kufungwa na vyombo vya habari kutishiwa.

Mrithi wake Samia Suluhu Hassan amerudi nyuma katika sera zake kadhaa zenye utata na kuahidi mageuzi yaliyotakwa na upinzani kwa muda mrefu.

Lakini matumaini yaliyoletwa na maamuzi hayo ya awali yalififishwa na kukamatwa mwezi Julai 2021 kwa kiongozi wa chama cha upinzani cha CHADEMA, Freeman Mbowe na maofisa watatu wa chama Mwanza (magharibi), ambako walipaswa kushiriki katika mkutano wa kudai marekebisho ya Katiba.

Baada ya kukamatwa huku, upinzani ulimwita rais "dikteta". Lakini baada ya miezi saba ya kesi ya "ugaidi", waendesha mashtaka hatimaye walitangaza mnamo Machi 2022 kufuta mashtaka dhidi ya watu hao wanne, kisha kuachiliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.