Pata taarifa kuu

M23 yapanga kujiondoa katika ngome zake Mashariki mwa DRC

Wakati shinikizo likiongezeka kuhusiana na mauaji ya Kishishe ambayo yamesababisha vifo vya watu 272, kulingana na serikali, kundi la waasi la M23 limetangaza kwa mara ya kwanza siku ya Jumanne uwezekano wa kujiondoa katika ngome zake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika kituo cha mpaka cha Bunagana nchini Uganda, Novemba 10, 2021 kufuatia mapigano makali kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa DRC.
Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika kituo cha mpaka cha Bunagana nchini Uganda, Novemba 10, 2021 kufuatia mapigano makali kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa DRC. AFP - BADRU KATUMBA
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo linaweza kuashiria mwanzo wa awamu mpya ya mzozo kati ya M23 na jeshi la DRC. Siku ya Jumanne Desemba 6, M23 ilisema iko "tayari kuanza kujiondoa", hata kama haikuwakilishwa kwenye mkutano mdogo wa kilele mjini Luanda wiki mbili zilizopita.

Kundi hili la waasi linaendelea kudai kuwa linaheshimu makubaliano ya usitishwaji wa mapigano, hata kama mapigano hayajaisha kabisa katika eneo la magharibi huko Rutshuru. Pia inasisitiza ombi lake la mazungumzo ya moja kwa moja na serikali ya DRC "kutafuta suluhu la kudumu kwa sababu ya mzozo wa mashariki mwa DRC" na inataka mkutano na jeshi la kanda ya Afrika Mashariki.

Tangazo hili linakuja katika muktadha wa shinikizo kali. Kwa siku chache zilizopita, mamlaka ya DRC imekuwa ikiwanyooshea kidole waasi wa kundi la M23 kufuatia mauaji ya Kishishe. M23 inakanusha tuhuma hizi. Pia linakuja baada ya mazungumzo ya simu kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken na Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Kama ukumbusho, wakati wa mkutano mdogo wa kilele huko Luanda, washiriki waliomba kusitishwa kwa mapigano, kisha kuondolewa taratibu kwa waasi wa kundi la M23 kwenye ngome zake. Awali kundi hili la waasi lilijibu kwamba halikuhusiki na taarifa hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.