Pata taarifa kuu

DRC yataka ICC kufungua uchunguzi kuhusu mauaji ya Kishishe

Mamlaka ya DRC inaitaka ICC kufungua uchunguzi kuhusu kile kilichotokea Kishishe mashariki mwa nchi hiyo siku ya Jumanne, Novemba 29. Siku ya Jumatatu, serikali ilitangaza watu 272 waliouawa. Mamlaka inawashutumu M23 kwa kushambulia wakaazi. Kinshasa inabaini kwamba itafikisha malalamiko yake mbele ya mahakama za kimataifa.

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) huko Hague, Novemba 23, 2015.
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) huko Hague, Novemba 23, 2015. AFP - MARTIJN BEEKMAN
Matangazo ya kibiashara

 

Rose Mutombo, Waziri wa Sheria wa DRC, yuko Jumanne hii huko Hague ambapo Mkutano wa 21 wa Nchi Wanachama unafanyika. Alizungumza asubuhi ya leo kwenye jukwaa. "Wakati tuko katika chumba hiki, sehemu ya eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini ni eneo linalokumbwa na uhalifu dhidi ya binadamu, uhalifu wa kivita, uhalifu wa mauaji ya kimbari na uhalifu wa uchokozi unaosababisha vifo vya maelfu ya watu, unyanyasaji wa kijinsia, bila kusahau maelfu yawatu kuyatoroka makaazi yao. "

Waziri aliomba washiriki katika mkutano huo kusalia kimya kwa dakika moja. Kuhakikisha kuwa wahalifu wanajulikana: ADF na M23, ambao anawataja kama "wasaidizi wa jeshi la Rwanda"

Wakati akikaribisha tangazo lililotolewa Jumatatu na Mwendesha Mashtaka wa Mahakama hiyo, Karim Khan, kutembelea baadhi ya nchi hivi karibuni, DRC, kupitia kwa rais wake Félix Tshisekedi, anaomba kwa sauti ya waziri kwa mwendesha mashtaka kuanzia ziara yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ziara hii itamuwezesha "kutambua maafa ya kibinadamu" ili "asisite" kuwakamata wahusika wote na washirika wao, washirika wa uhalifu mkubwa. "Zaidi ya hayo, kutokana na uchokozi ambao nchi yangu ni mwathiriwa kwa upande wa Rwanda, nina hakika kwamba itanufaika na dhulma kama zile jumuiya ya kimataifa inalalamikia kwa nchi ya Ukraine", amesisitiza Waziri Rose Mutombo.

Tangu kuibuka tena kwa waasi wa M23 mashariki mwa Kongo mnamo Novemba 2021, ICC haijatangaza uchunguzi wowote kuhusu vitendo ambavyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita au uhalifu dhidi ya binadamu. Katika mji huu wa Kishishe, uliyoko chini ya kilomita 100 kaskazini mwa mji wa Goma, mamlaka ya Kongo inazungumzia "mauaji".

Maombolezo ya kitaifa ya siku tatu yalimalizika jana Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.