Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

DRC: Jiji la Bunagana lina jumla ya miezi 2 chini ya udhibiti wa M23

Ni miezi miwili sasa, Jumamosi hii Agosti 13, tangu mji wa Bunagana (mkoa wa Kivu Kaskazini) kukaliwa na waasi wa kundi lliloanzishwa mwezi Machi (M23). Mashirika ya kiraia na mamlaka za mitaa katika eneo la Rutshuru wanasema wana wasiwasi kwamba kundi hili la waasi linaimarisha uwepo wake katika eneo hili.

Raia wa Kongo katika kituo cha mpaka cha Bunagana wakati M23 ilipowasili Juni 7, 2022.
Raia wa Kongo katika kituo cha mpaka cha Bunagana wakati M23 ilipowasili Juni 7, 2022. © BADRU KATUMBA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Miezi miwili baada ya uvamizi huu, kulingana na watu mashuhuri wa eneo hilo, waasi tayari wameweka utawala sambamba katika jiji hilo, ambapo umeteua viongozi wake na kutoza ushuru wa kila mwezi kwa wakaazi wachache ambao wamebaki katika mji huo.

Wakazi wa mji wa Bunagana wanatoa wiki kwa serikali kufanya juhudi zote ili kuwafukuza waasi hawa katika eneo hili, ili kuruhusu maelfu ya watu waliokimbia makazi yao, ambao wako katika dhiki, kurejea katika familia zao.

Bunagana ilikuwa kituo muhimu cha forodha kwa mapato ya mkoa huo. Mji wa Bunagana unapatikana zaidi ya kilomita 100 kaskazini mashariki mwa Goma, katika eneo la Jomba katika huko Rutshuru, kwenye mpaka na Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.