Pata taarifa kuu

Msumbiji: Zaidi ya watu 110,000 watoroka makazi yao baada ya mashambulizi ya wanajihadi

Mashambulizi ya hivi majuzi ya wanajihadi kaskazini mwa Msumbiji tayari yamesababisha zaidi ya watu 110,000 kuhama makazi yao, wakiwemo zaidi ya watoto 60,000, shirika lisilo la kiserikali la Save the Children limesema siku ya Jumanne.

Mlipuko mpya wa ghasia ulitokea kaskazini mwa Msumbiji takriban wiki mbili zilizopita, kulingana na vyanzo vya ndani na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), shirika la Umoja wa Mataifa.
Mlipuko mpya wa ghasia ulitokea kaskazini mwa Msumbiji takriban wiki mbili zilizopita, kulingana na vyanzo vya ndani na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), shirika la Umoja wa Mataifa. © MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Zaidi ya watoto 61,000 wamekimbia wimbi jipya la vurugu" katika jimbo la Cabo Delgado katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, shirika la misaada la Save the Children limesema katika taarifa.

Machafuko mapya yalizuka katika jimbo hili kabla ya Krismasi, na yanaendelea katika hali ya hapa na pale lakini endelevu, kulingana na vyanzo vya ndani na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM). Siku ya Jumatatu shirika hilo la Umoja wa Mataifa lilisema kwamba idadi ya watu waliokimbia makazi yao ilifikia 112,894 kwa kipindi cha kuanzia Desemba 22 hadi Machi 3. Maelfu ya familia walikimbia kwa basi, mitumbwi au kwa miguu.

Mwanasaikolojia kutoka Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF), Esperança Chinhanja, aliye katika jimbo hili maskini, ameonya kuhusu matokeo makubwa ya mashambulizi ya hivi majuzi dhidi ya afya ya akili. "Wasiwasi, mashambulizi ya hofu, kukosa usingizi, hisia za kutengwa na mawazo ya mara kwa mara: wengine pia hutaja mawazo ya kujiua," asema.

Tangu mwezi Oktoba 2017, jimbo hilo lenye utajiri wa gesi kaskazini mwa koloni la zamani la Ureno limekukumbwa na uasi unaoongozwa na wanajihadi wanaohusishwa na kundi la Islamic State (IS).

“Ripoti za mara kwa mara za kukatwa vichwa na utekaji nyara, ikiwa ni pamoja na waathiriwa vijana kadhaa,” limebanisha shirika hili la Save the Children, ilhali vita hivi vya msituni “havionekani kutoweka hivi karibuni.”

Kwa msaada wa maelfu ya wanajeshi kutoka Rwanda na nchi jirani za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) tangu mwaka 2001, serikali imepata tena udhibiti dhaifu katika sehemu kubwa ya jimbo hilo lakini mashambulizi ya wanajihadi yanaendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.