Pata taarifa kuu

Joe Biden amshambulia Donald Trump moja kwa moja katika hotuba kuu ya kampeni

Rais wa Marekani Joe Biden amemponda mpinzani wake Donald Trump siku ya Ijumaa usiku, Januari 5, katika hotuba yake kuu ambayo anatarajia kuipa nguvu kampeni yake ya uchaguzi wa urais mwezi Novemba.

Joe Biden amechukua hatua ya kuzindua upya kampeni yake kwa hotuba hii huko Pennsylvania, Ijumaa Januari 5.
Joe Biden amechukua hatua ya kuzindua upya kampeni yake kwa hotuba hii huko Pennsylvania, Ijumaa Januari 5. AP - Stephanie Scarbrough
Matangazo ya kibiashara

Mahali alipotolea hotuba yake palichaguliwa kama ishara. Valley Forge, Pennsylvania, ilimwona George Washington, rais wa kwanza mtarajiwa wa Marekani, akikusanya vikosi vya kijeshi vya Marekani vilivyopigana dhidi ya Milki ya Uingereza karibu miaka 250 iliyopita. Kwa hivyo ni kwenye eneo hili la kihistoria ya Vita vya Uhuru wa Marekani, ndipo ambapo Joe Biden alianza kumponda mpinzani wake Donald Trump katika hotuba ambayo anatumai itakuwa ya maamuzi kwa muda wote wa kampeni yake.

Rais huyu wa zamani wa Marekani, anayepewa nafasi kubwa ya kutetea chama cha Republican katika uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba, "yuko tayari kufidia demokrasia yetu ili kupata mamlaka", Joe Biden alimuandama hivyo Donald Trump. "Anazungumza juu ya damu ya Wamarekani kuwekewa sumu, kwa kutumia lugha sawa na ambayo ilitumiwa nchini Ujerumani chini ya utawala wa Kinazi," ameongza Joe Biden, 81, ambaye anakaribiana kura na Donald Trump katika tafiti za hivi karibuni.

Rais alipangiwa kutoa hotuba yake Jumamosi hii, miaka mitatu baada ya shambulio la Capitol lililofanywa na wafuasi wa Donald Trump ambao walijaribu kuzuia kuthibitishwa kwa ushindi wa Joe Biden, lakini tarehe hiyo iliondolewa kutokana na utabiri wa kimbunga. Shambulio dhidi ya Capitol bado ni suala la mzozo nchini Marekani: robo ya Wamarekani wanaamini, bila uthibitisho, kwamba FBI ilikuwa chanzo, kulingana na utafiti wa Gazeti la Washington Post na Chuo Kikuu cha Maryland iliyotolewa wiki hii.

"Trump na wafuasi wake wa MAGA ("Make America Great Again", kauli mbiu ya bilionea wa chama cha Republican) sio tu kwamba wanaunga mkono vurugu za kisiasa, lakini wanacheka kuhusu hilo," ameshutumu Joe Biden. Msemaji wa Trump, Steven Cheung, mara moja amejibu kwamba Biden alikuwa "tishio la kweli kwa demokrasia."

Mwanzo mgumu wa kampeni

Nia hii ya kuharakisha kampeni ya Joe Biden inakuja baada ya ukosoaji kutoka kwa baadhi ya Wanademokrasia ambao wanaamini kuwa ilianza polepole sana. Rais alishindwa kuwashawishi wapiga kura kuwa uchumi ulikuwa ukiimarika licha ya idadi ya kazi bora kuliko ilivyotarajiwa siku ya Ijumaa, huku bei zikisalia "bado ni za juu sana kwa Wamarekani wengi," amekiri katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Changa moto nyingine kwa upande wa Demokrasia: uhamiaji na suala la mpaka wa Mexico, kuunga mkono vita vya Israel dhidi ya Hamas ambavyo vinagawanya chama chake au hata Congress ambayo inazuia ombi lake la kuongezewa fedha kwa Ukraine. Kukataa kwa Joe Biden kutaja kesi nyingi za kisheria za Donald Trump, ili kutotoa hisia ya kushawishi mfumo wa mahakama, pia kulimnyima moja ya silaha zake kuu dhidi ya bilionea huyo wa chama cha Republican.

Lakini dosari ya kwanza ya Joe Biden labda inabaki kuwa umri wake. Mitelezo na makosa yake machache ya lugha yanachunguzwa. Ana kiwango kibaya zaidi cha umaarufu kwa rais aliyeko madarakani mwezi wa Desemba kabla ya uchaguzi.

Klipu ya kwanza ya kampeni ya Joe Biden iliyotolewa Alhamisi na ambayo itarushwa kwa mara ya kwanza kwenye runinga Jumamosi inaonya juu ya tishio "kali" kwa demokrasia kwa kutangaza picha za shambulio la Capitol mnamo Januari 6, 2021. " Lilikuwa jambo la kutisha kuona,” msemaji wa Ikulu ya White House Karine Jean-Pierre aliwaambia waandishi wa habari siku ya Alhamisi. “Rais ataendelea kuongea na kulizungumzia hilo. "

(Na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.