Pata taarifa kuu
USALAMA-MAANDAMANO

Haiti: Waandamanaji kadhaa dhidi ya kundi lenye silaha wauawa Port-au-Prince

Waumini kadhaa wa kanisa la kiinjili nchini Haiti, ambao waliandamana karibu na kiongozi wao dhidi ya kundi moja lenye silaha kudhibiti eneo moja la mji wa Port-au-Prince, waliuawa kwa kupigwa risasi Jumamosi, polisi imesema, na kuongeza kuwa wengine walitekwa nyara au kujeruhiwa.

Kundi la watu wenye silaha limewaua waumini kadhaa wa kanisa la Kiinjili katika moja ya maeneo ya mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince.
Kundi la watu wenye silaha limewaua waumini kadhaa wa kanisa la Kiinjili katika moja ya maeneo ya mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince. © RICHARD PIERRIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Idadi rasmi ya mauaji hayo haijajulikana, eneo hilo linadhibitiwa na kundi lenye silaha la Canaan, mojawapo ya makundi yanayoendesha uhalifu katika vitongoji vingi vya mji mkuu wa Haiti.

Mapanga na vijiti dhidi ya silaha za kivita

Maandamano hayo yaliandaliwa na Mchungaji Marco Zidor, kiongozi wa Kanisa la kiinjili la Piscine de Bethesda. Mtu huyo anayejionyesha kuwa ni mganga, aliwakusanya wafuasi wake, wengine wakiwa wamebeba panga au fimbo, ili waandamane kuelekea eneo linaloshikiliwa na kundi lenye silaha la Canaan.

Hata hivyo washambuliaji, walifyatua risasi wakati umati ulipofika katika eneo hilo wanalodhibiti. Kwenye video zilizosambazwa na kundi hilo, kunaonekana maiti nyingi zikiwa zimetapakaa chini.

Alipohojiwa na shirika la habari la AFP, afisa wa kanisa la kiinjili la Piscine de Bethesda amebaini kwamba "hayuko katika nafasi nzuri ya kutoa habari kwa sasa".

Uchunguzi wafunguliwa na polisi

Polisi ya Haiti, kwa upande wake, inasema imefungua uchunguzi na kulaani "tukio la kusikitisha" siku ya Jumatatu, ikidai kujaribu kuzuia umwagaji damu, bila mafanikio.

Mwanamume akshikilia panga wakati wa maandamano ya kupinga ukosefu wa usalama huko Port-au-Prince, Agosti 25, 2023.
Mwanamume akshikilia panga wakati wa maandamano ya kupinga ukosefu wa usalama huko Port-au-Prince, Agosti 25, 2023. AP - Odelyn Joseph

“Jeshi la Polisi lilikuwa limechukua hatua kwa kutenga eneo la usalama ili kuwazuia washiriki kufika wanakoenda, na kuanza mazungumzo kwa nia ya kuwashawishi waandaaji wasiendelee na shughuli hii ili kuepusha mauaji ya majambazi ambao wana silaha za kivita. ," polisi imesema katika taarifa.

"Hata hivyo, waandamanaji walipuuza mipango ya usalama ambayo iliwekwa na vikosi vya usalama, na walifika katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi lenye silaha," polisi imeongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.