Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Haiti: Thelathini waangamia katika shambulio dhidi ya moja ya mitaa ya Port-au-Prince

Watu 30 wamefariki wakiwemo maafisa wawili wa polisi katika shambulizi la watu wenye silaha dhidi ya wakaazi wa mtaa mmoja katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince. Pia watu wanne hawajulikani walipo na makumi kujeruhiwa, kulingana na ripoti ya muda ya shirika moja la haki za binadamu. 

Marekani inataka kusaidia kudumisha amani nchini Haiti kupitia jeshi la kimataifa.
Marekani inataka kusaidia kudumisha amani nchini Haiti kupitia jeshi la kimataifa. © RICHARD PIERRIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya wakaazi wamelazimika kutoroka makaazi yao kufuatia shambulio la kundi la watu wenye silaha lililogharimu maisha ya watu 30 na makumi kujeruhiwa katika eneo la Carrefour-Feuilles, moja ya mitaa ya Port- au-Prince, linalokumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara.

Tangu Jumanne Agosti 15, maelfu ya wakazi wamekimbia eneo la Carrefour-Feuilles, mtaa wa kimkakati kwa makundi yenye silaha, ambayo yanadhibiti sehemu kubwa ya nchi hii maskini inayokabiliwa na na ukosefu wa usalama.

Watu 30 wamefariki wakiwemo maafisa wawili wa polisi katika shambulizi la watu wenye silaha dhidi ya wakaazi wa mtaa mmoja katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince. Pia watu wanne hawajulikani walipo na makumi kujeruhiwa, kulingana na ripoti ya muda ya shirika moja la haki za binadamu. Tangu Jumanne Agosti 15, maelfu ya wakazi wamekimbia eneo la Carrefour-Feuilles, mtaa wa kimkakati kwa makundi yenye silaha, ambayo yanadhibiti sehemu kubwa ya nchi hii maskini inayokabiliwa na na ukosefu wa usalama.

Kundi linalohusika naa shambulio hilo, likiongozwa na Renel Destina (au Ti Lapli), limepora mali na vutu na kuchoma nyumba. Baadhi ya wahanga wameuawa kwa silaha za kivita. Ripoti ya ghasia za Carrefour-Feuilles imetolewa kwa shirika la habari la AFP na Mtandao wa Kitaifa wa Kutetea Haki za Kibinadamu (RNDDH). "Takwimu hizi zilikusanywa baada ya ushuhuda wa wazazi kutoka kwa ndugu wa wahanga ambao tulikutana nao", amesema mkurugenzi mtendaji wa RNDDH, Pierre Espérance.

Watu 5,000 watoroka makaazi yao

Dominique Charles, mmoja wa wakaazi wa eneo hilo, ameliambia shirika la AFP kwamba amepoteza mama yake, baba mkwe wake, mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 18, dada zake wawili na kaka yake katika mashambulizi haya. "Washambuliaji walishambulia nyumba yetu kwa mabomu yaliyotengenezwa kienyeji. Niliweza kutoroka lakini wanafamilia wengine hawakupata fursa hii”, amesema alipokuwa akija kutoa ushahidi katika makao makuu ya RNDDH.

Tangu mwanzoni mwa wiki, ghasia hizi zimesababisha zaidi ya watu 5,000 kutoroka makaazi yao kulingana na Jerry Chandler, mkurugenzi mkuu wa kikosi cha ulinzi wa raia nchini Haiti. Waliondoka Carrefour-Feuilles kwa miguu, kwa pikipiki au kubanana ndani ya magari. Miongoni mwao, "wanawake, watoto, wazee", ameeleza Jerry Chandler.

Maelfu haya ya waliokimbia makazi yao wamepata hifadhi katika shule au kituo cha michezo, wengine mitaani. Siku ya Alhamisi mamlaka ilitangaza kwamba wameanza kusambaza chakula cha moto na maji ya kunywa kwa waathiriwa.

Haiti imekwama kwa miaka mingi katika mzozo mkubwa wa kiuchumi, usalama na kisiasa, ambao umeimarisha umiliki wa magenge. Magenge haya yenye silaha yanadhibiti takriban 80% ya mji mkuu wa Haiti na uhalifu wa vurugu ni wa mara kwa mara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.