Pata taarifa kuu

Colombia: Raundi ya nne ya mazungumzo kati ya Bogota na waasi wa ELN kuanza

Duru ya nne ya mazungumzo kati ya serikali ya Colombia na waasi wa mwisho wa nchi hiyo, Jeshi la Ukombozi la Kitaifa (ELN) yanaanza leo Jumatatu Agosti 14. Tangu Agosti 3, usitishaji mapigano wa kihistoria ulianzishwa kati ya pande hizo mbili, ikiwa ni tukio la kwanza la kihistoria ambalo si rahisi kama ilivyokuwa ikitarajiwa. Tangu mwanzo, kashfa za kisiasa na mashambulizi yamekuwa yakitatiza mazungumzo kuendelea. Mazungumzo haya yanatarajia kuanza katika mazingira magumu.

Aliyekuwa mwasi wa M-19 Otty Patiño, kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Colombia katika mazungumzo na kundi la waasi la ELN, huko Bogota mnamo Julai 28, 2023.
Aliyekuwa mwasi wa M-19 Otty Patiño, kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Colombia katika mazungumzo na kundi la waasi la ELN, huko Bogota mnamo Julai 28, 2023. AFP - DANIEL MUNOZ
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu nchini Colombia, Najet Benrabaa

Kuanza tena kwa mazungumzo hayo kunakuja wiki moja baada ya moja ya kashfa muhimu za kisiasa nchini humo, ile ya kukamatwa kwa mtoto mkubwa wa rais kwa utakatishaji fedha, lakini pia kutokana na madai ya mpango wa mauaji dhidi ya mwendesha mashtaka yaliyohusisha waasi.

Matukio haya mawili yanadhoofisha taswira na uaminifu, kwa upande mmoja, kwa Rais Gustavo Petro, na kwa upande mwingine, kwa ujumbe wa waasi ambao utakuwa kwenye meza ya mazungumzo nchini Venezuela huko Caracas siku ya Jumatatu.

Licha ya hayo, usitishaji vita wa miezi sita unaendelea. Tume za kufuatilia na kutathmini utekelezaji wake zimeundwa. Tume hizo zinapaswa kufanya iwezekane kupunguza mivutano na kusaidia kufungua mazungumzo zaidi kuelekea kumalizika kwa mzozo wa silaha.

Kwa vyovyote vile, ni matarajio ya rais wa mrengo wa kushoto Gustavo Petro, ambaye anaweka dau mkakati wake wote wa amani kamili juu ya mafanikio ya mazungumzo haya na wapiganaji wa mwisho wa msituni nchini humo. ELN bado ina maelfu ya wapiganaji. Mapambano yake ya silaha yamekuwa yakiendelea kwa karibu miaka 60.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.