Pata taarifa kuu

Colombia: EMC, upinzani wa Farc, 'tayari' kuanza mazungumzo ya amani

Waasi wa FARC (EMC-FARC), wapinzani wakuu wa Kikosi cha Wanajeshi wa Mapinduzi ya Colombia (FARC),walmesema wako "tayari", Jumapili hii wakati wa mkutano wa hadhara kusini mwa Colombia, kuanza mazungumzo ya amani na serikali mwezi ujao.

Nchini Colombia, mazungumzo ya amani yaliyoanzishwa na Rais wa mrengo wa kushoto Gustavo Petro (kwenye picha) yanaendelea kadri iwezekanavyo.
Nchini Colombia, mazungumzo ya amani yaliyoanzishwa na Rais wa mrengo wa kushoto Gustavo Petro (kwenye picha) yanaendelea kadri iwezekanavyo. REUTERS - LUISA GONZALEZ
Matangazo ya kibiashara

"Tunautangazia ulimwengu mzima kwamba wajumbe wetu kwenye meza ya mazungumzo na serikali wako tayari kwa Mei 16," msemaji wa "The Central General Staff" (Estado Mayor Central - EMC), kundi ambalo lilikataa kutia saini makubaliano ya Amani ya kihistoria ya mwaka 2016 kati ya Bogota na wapiganaji FARC, kundi ambalo walitokea.

Mnamo mwezi Septemba 2016, wapiganaji mia chache kutoka FARC (Majeshi ya Wanamapinduzi ya Colombia) walikataa kutia saini mkataba wa amani na kusalimisha silaha zao. Wanajiita leo "The Central General Staff" (Estado Mayor Central - EMC) na wana wapiganaji wenye silaha zaidi ya 3,000, waliotumwa hasa kwenye pwani ya Pasifiki, kwenye mpaka na Venezuela na kusini mwa nchi. Chini ya amri ya "Ivan Mordisco" , ambaye jeshi lilitangaza kumuua mnamo mwezi Julai 2022, EMC wameshiriki katika miezi ya hivi karibuni katika mapigano mengine katika maeneo matatu nje ya Caqueta, ngome ya kihistoria ya waasi wa FARC.

'Jukwaa' kubwa la EMC huko San Vicente del Caguan

Tangu mwanzoni mwa mwezi huu, viongozi wa kijeshi wa EMC wamekuwa wakikutana katika eneo la San Vicente del Caguan, moja ya ngome za kihistoria za FARC - wakisema - kusikiliza wakazi wa eneo hilo na kufafanua msimamo wa pamoj , anaripoti mwandishi wetu huko Bogotá, Marie-Eve Detoeuf. Kundi hili linaandaa mkutano mkubwa Jumapili hii na "jamii", "walinzi wa wakulima" na mashirika mengine ya vijijini katika maeneo haya chini ya udhibiti wa waasi, linabainisha shirika la habari la AFP ambalo limealikwa kwenye mkutano. "Jamii zilitualika kufafanua mchakato unaoendelea (wa amani) na serikali," amesema Kamanda Andrey Avendano.

Kwa kumbukumbu, kwa mpango wa Rais wa mrengo wa kushoto Gustavo Petro, usitishaji vita wa miezi sita umefikiwa tangu Januari 1 na makundi kadhaa yenye silaha yakiwemo ELN (Jeshi la Ukombozi la Kitaifa), makundi makuu ya upinzani yaa FARC na makundi mengine yenye silaha yanayohusishwa na biashara ya madawa ya kulevya. Ilikuwa ni moja ya ahadi za kampeni za rais mpya wa Colombia. Usitishaji mapigano ambao umeshuhudia ukiukwaji kadhaa, kama ilivyokuwa kwa ELN mnamo mwezi Machi.

Katikati ya wiki iliyopita, serikali ilitangaza kuwa mchakato wa amani na EMC-FARC  'unaendelea'. Mkutano ulifanyika mnamo Aprili 12, mbele ya wawakilishi wa jumuiya ya kimataifa, na makamanda wapatao kumi na tano wa kundi hili walikusanyika katika eneo la San Vicente del Caguan (kusini-magharibi). Mahakama ya Colombia imesimamisha hati ya kukamatwa kwa viongozi 19 wakuu wa waasi wa EMC-FARC.

Lakini mijadala hii haizuii makabiliano ya mara kwa mara na jeshi. Siku ya Ijumaa Aprili 14, waasi hao walishutumu ukiukaji wa usitishaji mapigano, hasa Aprili 11 na 12, mtawaliwa katika maeneo ya Cauca (kusini-magharibi) na Arauca (kaskazini mashariki). Makabiliano ya Aprili 11 yalisababisha vifo viwili katika safu yake .

Licha ya mvutano huu, viongozi wa kijeshi wa EMC-FARC walithibitisha Jumamosi kwamba "vitengo vyote vya kundi hili vimeelezea nia yao ya amani kwa maslahi ya raia". EMC-FARC inapendekeza kwa serikali kufanya mkutano nchini Norway.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.