Pata taarifa kuu
AMANI-MAZUNGUMZO

Joe Biden azuru Ireland Kaskazini kusherehekea amani na kuhimiza mazungumzo

Rais wa Marekani yuko nchini Jamhuri ya Ireland ambako atafanya siku mbili katika ziara yake ya kiserikali. Joe Biden ameambatana katika ziara yake hiyo na viongozi mbalimbali nchini.

Rais Joe Biden ashuka ndege ya Air Force One kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Belfast , Ireland Kaskazini, Jumanne, Aprili 11, 2023.
Rais Joe Biden ashuka ndege ya Air Force One kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Belfast , Ireland Kaskazini, Jumanne, Aprili 11, 2023. AP - Patrick Semansky
Matangazo ya kibiashara

Bila shaka angependa kusherehekea amani isiyo na bugdha, lakini anafika katikati ya mdororo wa kisiasa, na katika hali ya mvutano: Joe Biden anafanya ziara nchini Ireland Kaskazini, ambapo atajaribu kuhimiza mazungumzo.

Kipaumbele cha Joe Biden ni "kudumisha amani" ambayo ilikuwa ni vigumu kuijadili miaka ishirini na mitano iliyopita huko Ireland Kaskazini.

Siku ya Jumanne msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa kwenye ikulu ya White House, John Kirby, aliwaambia waandishi wa habari kwamba  Biden anajali Ireland Kaskazini na ana historia ndefu ya kuunga mkono amani na ustawi wa eneo hilo.

Hivi leo Jumatano, Joe Biden anatarajia kutoa hotuba katika chuo kikuu cha Ulster mjini Belfast, itakayoashiria mafanikio makubwa tangu kusainiwa kwa makubaliano hayo ya Ijumaa Kuu, mnamo mwaka 1998.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.