Mlipuko katika kituo cha mafuta waua takriban watu 9 nchini Ireland
Mkazi wa eneo hilo ambaye nyumba yake iko takriban mita 150 kutoka eneo la tukio amesema mlipuko huo ulimfanya afikirie kuwa ni "bomu".
Imechapishwa:
Takriban watu tisa waliuawa katika mlipuko uliotokea katika kituo cha mafuta katika kijiji kimoja kaskazini magharibi mwa Ireland ambapo zoezi la kuwatafuta waathiriwa umeendelea siku ya Jumamosi.
Ijumaa alaasiri Polisi ilitangaza idadi ya watu waliouawa imeongezeka kutoka saba hadi tisa. "Shughuli ya kuwatafuta waathiriwa wengine zinaendelea," iliongeza. Watu wanane walilazwa hospitalini.
Polisi, hata hivyo, haikutoa maelezo juu ya asili ya mlipuko huu, uliotokea Ijumaa alasiri katika kijiji cha Creeslough.