Pata taarifa kuu

Washington yataka washawishi kwenye TikTok kupambana na taarifa potofu kuhusu Ukraine

Jinsi gani ya kufanya mamilioni ya vijana kuelewa vigingi vya vita vya Ukraine wakati hawasomi taarifa zinazotolewa kwenye magazeti au kutazama taarifa za habari katika televisheni au kuzikiliza taarifa za habari kwenye Redio?

Tangu kuzuka kwa mzozo nchini Ukraine, TikTok imejawa na habari kuhusu Ukraine. Hapa, nembo ya jukwaa la TikTok Februari 15, 2022.
Tangu kuzuka kwa mzozo nchini Ukraine, TikTok imejawa na habari kuhusu Ukraine. Hapa, nembo ya jukwaa la TikTok Februari 15, 2022. © Dado Ruvic, Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na umuhimu uliochukuliwa hasa na jukwaa la TikTok, lililojaa video za vita, Washington sasa inawatolea wito washawishi "kuwafahamisha" wakati wa mikutano na waandishi wa habari, kama ilivyo kwa waandishi wa habari wenye taaluma. Hii ni kwa matumaini ya kufikia mamilioni ya waliojisajili, wanaojulikana kupenda video za mtandaoni na zilizorahisishwa.

Kwenye mtandao wa TikTok, anajieleza kama "mwanahistoria wa kizazi Z": Kahlil Greene, umri wa miaka 21 na wanaomfuata 550,000 kwenye jukwaa, aakiwa amesimama mbele ya picha ya Ikulu ya White House, kama vile wachambuzi wa masuala ya kijiografia wa vituo maarufu vya televisheni. Yeye ni mmoja wa washawishi 30 wa TikTok ambao walialikwa kwa muhtasari kwa njia ya video na utawala wa Biden siku chache zilizopita, ameripoti mwandishi wetu wa New York, Carrie Nooten.

Kama vile Aaron Parnas, ambaye tangu wakati huo amekuwa chanzo kikuu cha habari kwa watu milioni 1.2: akiwa na miaka 22, hutoa video kila baada ya dakika 45, kutoka saa tatu asubuhi hadi saa nne usiku. - ana familia nchini Ukraine na vyanzo vyake vya moja kwa moja ni waandishi wa habari na vyombo vya habari vya Ukraine.

Aaron Parnas mara moja alishiriki na wafuasi wake kile Washington ilikuwa ikifanya kuisaidia Ukraine. Miongoni mwa mambo mengine, "Marekani inatenganisha na kufichua kiasi kikubwa cha habari zilizoainishwa ili kukabiliana na taarifa potofu za Urusi, na kujulisha umma na Ukraine kuhusu kile kinachotokea huko".

Hii sio mara ya kwanza kwa Ikulu ya White House kutegemea washawishi wa mtandao waTikTok kufikisha ujumbe wake, kwani tayari ilikuwa imewahamasisha wakati wa kampeni ya chanjo dhidi ya Covid-19. Na mbali na kufikiria kuwa wanaweza kuwa chombo cha propaganda: Vijana wa kizazi hiki kilichopewa jina la Z wanakariri kwamba zaidi ya yote inawawezesha kusambaza habari za moja kwa moja kwa watazamaji ambao hawajafahamishwa na vyombo vya habari kwa muda mrefu.

"TikTok ina jukumu muhimu"

"TikTok ina jukumu muhimu, kwa sababu hapo ndipo wengi wa kizazi kipya hupata habari," kulingana na Chris Dier, mwalimu wa historia wa shule ya upili ya New Orleans.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.