Pata taarifa kuu

Ukraine: Mashambulizi yaenea hadi Magharibi, kambi ya kijeshi yashambuiwa karibu na Lviv

Katika siku ya kumi na nane ya uvamizi wa Ursi nchini Ukraine, Jumapili Machi 13, Kiev inajiandaa kupigana, wakati mji wa Mariupol unatarajia kupokea msaada. Wakati huo huo milipuko ya mabomu inaendeea kusikika Magharibi mwa nchi, karibu na mpaka wa Poland.

Mwanajeshi akiwa mbele ya lango la hospitali baada ya shambulio kwenye kituo cha kijeshi cha Yavoriv nchini Ukraine, Machi 13, 2022.
Mwanajeshi akiwa mbele ya lango la hospitali baada ya shambulio kwenye kituo cha kijeshi cha Yavoriv nchini Ukraine, Machi 13, 2022. © REUTERS/Kai Pfaffenbach
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Kwenye uwanja wa vita, kambi ya kijeshi huko Magharibi, karibu na mpaka wa Poland, imeshambuiwa Jumapili asubuhi. Mashambulizi hayo, ambayo yamelenga kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Yavoriv, ​​yamesababisha vifo vya makumi ya watu.

► Vikosi vya Urusi bado vinajaribu kuizingira mji wa Uraine Kiev. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameahidi "kukabiiana na mashambulizi"yoyote dhidi ya mji huo.

► Kusini mwa nchi, shambulio la bomu limeua watu kadhaa huko Mykolaiv mapema Jumapili, hatua ya mwisho kabla ya bandari ya Odessa. Mji wa Mariupol, ambao bado umezingirwa, ulikuwa unajianda siku ya Jumamosi kupokea msafara wa msaada wa kibinadamu ambao ulikuwa umezuiliwa kwa zaidi ya miaka mitano katika kituo cha ukaguzi cha vikosi vya Urusi.

► Kwa upande wa kidiplomasia, Emmanuel Macron na Olaf Scholz walizungumza na Vladimir Putin siku moja baada ya mkutano wa kilele wa Versailles. Wito wao wa kusitishwa kwa mapigano haujasikilizwa, huku rais wa Urusi akishutumu vikosi vya Ukraine kwa "ukiukaji wa wazi" wa sheria za kibinadamu. Mdai ya "uongo", ofisi ya rais wa Ufaransa imejibu.

► Rais wa Ukraine amebaini kuwa takriban wanajeshi 1,300 wa Ukraine wamefariki tangu kuanza kwa mashambulizi ya Urusi.

Kufikia sasa watu 2, 698, 280 wameitoroka Ukraine, kufuatia uvamizi wa Urusi, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumoia wakimbizi, UNHCR.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.